JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SACCOS TUMIENI MIFUMO YA KIDIGITALI - NAIBU WAZIRI SILINDE

Share This
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde ametoa wito kwa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo(SACCOS) kuendelea kutumia mifumo ya Kidigitali mbalimbali iliyopo sokoni inayoendana na uwezo wa Kifedha wa SACCOS ikiwemo mfumo ulioandaliwa na unaondeshwa na Muungano wa SACCOS nchini (SCCULT).

Ameeleza Mhe Silinde Mfumo huu umeandaliwa kwa mazingira ambayo ni rafiki na unaoendana na mahitaji ya SACCOS Nchini na SCCULT itatimiza jukumu lake na itawasimamia vema kwenye suala hili.

Ameeleza hayo leo tarehe 21/10/2024 wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani, yanayofanyika jijini Mwanza yenye kauli mbiu “Ulimwengu Mmoja Kupitia Ushirika wa Kifedha”

Mheshimiwa Silinde ameeleza Matumizi ya TEHAMA ni lazima kama Vyama vinataka kuendelea kuwahudumia wanachama vema na kuhimili ushindani uliopo kwenye soko la fedha na muendele kutumia mfumo wa MUVU katika uendeshaji na usimamizi wa shughuli za vyama.

“Umefika wakati sasa kuacha kabisa kujiendesha kwa mazoea na kutumia makaratasi, nafahamu kumekuwepo na mazoea ya kupuuza kwa makusudi maelekezo na ushauri unaotolewa ili kukuza sekta na kuboresha utendaji wa SACCOS zenu” amesema Mhe. Silinde.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya SCULLT, Khajat Aziza Mshana, amesema Maadhimisho haya yanafanyika kwa mara ya 76 Ulimwenguni tangu kuanzishwa kwake na mara ya 15 kwa Tanzania na SACCOS zimekuwa na nguvu na ushawishi wa kuunganisha jamii kwa kutoa Huduma ambazo zinagusa na kubadilisha maisha ya wanachama na jamii kwa ujumla.

Naye Mrajis na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, ameeleza Tume imepokea maombi 1,211 ya Leseni kutoka kwa SACCOS na ilikuwa imetoa Leseni 963 kwa SACCOS zilizokidhi sifa na vigezo vya kupewa Leseni hizo kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Huduma Ndogo za Fedha.

“Niwaelekeze Viongozi wa SACCOS kuendelea kutekeleza vyema matakwa ya Sheria, Kanuni na Miongozo inayotolewa na ofisi kwa kufanya Mikutano Mikuu ya Mwaka na kuwasilisha Bajeti za SACCOS hizo mapema na muendele kufungua matawi na milango ya huduma kwa mujibu wa Sheria na mfahamu kosa la jinai kuendesha shughuli za matawi na milango ya huduma pasipo kuidhinishwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika” amesema Dkt. Ndiege.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad