JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


NMB WAWAFUNDA MIONO PWANI

Share This

 



Na Khadija Kalili Michuzi Tv
MENEJA  wa Matawi yote ya Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Seka Urio amehamasisha wanakijiji wa Kikarokuchagamkia fursa ya kupata mikopo yenye kujali heshima ya wateja inayotolewa na Benki hiyo .


Meneja huyo wa Matawi yote ya NMB Dar es Salaam na Pwani Urio amsema hayo wakati akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi katika Kijiji Cha Kikaro kilichopo Miono Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.


"NMB tunatoa mkopo fasta wa kiasi cha Mil.1 unaopatikana bila ya dhamana yoyote, hakuna kujaza makaratasi wala kutembelea tawi lolote hii ni fursa nzuri kwa wananchi ambayo tumewaletea Watanzania na marejesho yake ni ndani ya siku 7 hadi 28.


"Unaweza kushikwa na dharura na namnaya kupata mkopo huu mteja anatakiwa awe na akaunti inayofahamika kwa jina la Pesa Account ambayo haina makato yoyote huku mteja ataimiliki kwa kutumia simu yake ya kiganjani ya aina yeyote" amesema Urio.

"Lengo la kuanzishwa kwa Akaunti hii ni kumkomboa mwananchi katika mikopo umiza,kausha damu na mikopo mingineyo ambayo isiyozingatia utu wa mtu" amesema Urio.


Ameongeza kwa kusema kuwa akaunti hiyo ya mkononi imelenga kumsaidia mwananchi kutunza fedha zake.

Wakati huohuo wanafunzi wa Sekondari ya Kikaro iliyopo Miono wamepatiwa elimu ya kujiwekea akiba kwa kufungua akaunti inayofahamika kama Chipkizi Akaunti ambapo mwananfunzi atakuwa na kadi na kuweza kufanya miamala huku taarifa zotezikienda kwa mzazi na mwisho wa kutoa ni 50,000.
"Lengo la kuanzishwa kwq Akaunti ya Chipkizi ni kumuadaa mtoto kuwa na tabia ya kujiwekea akiba jambo ambalo vijanawa zamani hawakupatiwa hii elimu.

Urio ameongeza kwa kusema kuwa NMB wamejiwekea mkakati wa kupeleka wakala katika kila kijiji nchini ikiwa ni katika kuwapunguzia wananchi kutembea muda mrefu kufuata huduma za kifedha.

"Tunachagiza wananchi kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba kwa kupitia simu zao za mkononi na watapata taarifa zao zote za miamala iliyoingia na kutoka pamoja na kujiwekea akiba.
Baadhi ya wanakijiji wa Kikaro wakipatiwa semina na Maafisa wa NMB

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad