JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MAJALIWA: RAIS DKT. SAMIA ANAMATUMAINI MAKUBWA NA TAIFA STARS

Share This

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mazoezi ya timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (TAIFAR STARS) kwenye uwanja wa TRA , Mivinjeni jijini Dar es salaam, Oktoba 7, 2024. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (TAIFAR STARS) kwenye uwanja wa mazoezi wa TRA , Mivinjeni jijini Dar es salaam, Oktoba 7, 2024. 
Wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (TAIFA STARS) wakifanya mazoezi mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa TRA, Mivinjeni jijini Dar es salaam, Oktoba 7, 2024.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameitembelea Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) inayofanya mazoezi kwenye uwanja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassaan anamatumaini makubwa kuwa timu hiyo itafanya vizuri kwenye michezo yote miwili.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 07, 2024) alipozungumza na wachezaji, benchi la ufundi pamoja na viongozi wakiwa katika maandalizi ya michezo miwili ya kufuzu michuano ya AFCON 2025 dhidi ya Congo itakayochezwa Oktoba 10 na 15, 2024.

“Kila mmoja aone ana jukumu kubwa, kwako wewe mwenyewe na kwa nchi yako, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia anawatakia kila la kheri na alichofanya ametoa usafiri wa uhakika wa ndege itakayowapeleka nchini Congo kwa ajili ya mchezo wa Oktoba 10, 2024, hili ni jambo kubwa.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kwa jitihada za Rais Dkt. Samia amefanikiwa kushawishi mashirikisho ya mpira wa miguu ya Afrika na FIFA ili kuiona Tanzania ni nchi ambayo imeamua kuboresha viwango vya michezo ikiwemo mpira wa miguu. “Tumeanza kuona heshima tunayoipata ya kuwa wenyeji wa baadhi ya mashindano ikiwemo CHAN.”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wachezaji hao kushikamana, kuzungumza lugha moja na kutanguliza uzalendo. “Tumieni fursa ya imani ya Watanzania kwenu kuiwakilisha vyema Tanzania kwenye michezo iliyo mbele yenu.”

Kwa upande wake, Nahodha wa timu hiyo Mohammed Hussein “Tshabalala” amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwezesha kupatikana kwa usafiri wa ndege kwa ajili ya mchezo dhidi ya Congo. “Kwetu sisi hii ni motisha kuelekea michezo yetu miwili dhidi ya Congo, kwasababu itatusaidia kurejea haraka nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad