JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KAMPUNI ya Azam Media Group imezindua kampeni maalumu inayojulikana kama 'MENU IMEKAMILIKA'

Share This

 KAMPUNI ya Azam Media Group imezindua kampeni maalumu inayojulikana kama 'MENU IMEKAMILIKA'


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo leo Oktoba 10,2024 Bunju jijini Dar Es Salaam Meneja Mawasiliano na Mahusiao wa Azam Media, Christinah Korosso, amesema kupitia kampeni hiyo wanalenga kuboresha zaidi huduma kwa wateja wao.

Amesema miongoni mwa maboresho hao ni pamoja na kuhakikisha wateja wake wanapata maudhui ya kiwango cha juu zaidi.

"Na kampeni yetu hii maarufu kama Menu Imekamilika, itaboreshwa zaidi kwa kuhakikisha inaonyesha kila kitu kuanzia michezo, tamthilia, mfululizo wa vipindi na chaneli za watoto," amesema Christinah.

Grolia Chuwa ni Meneja Masoko wa Azam Media, amesema kwa sasa maboresho mengine wanayolenga ni kwenye michezo hususani ligi za La Liga Bundesliga, NBC na nyinginezo.

"Hivi karibuni tunenda kuanzisha mashindano ya ligi za nje (Laliga) na ligi zingine za nchi za nje ambapo mteja wetu ataweza kujishindia vitu mbali mbali ikiwemo kushinda safari ya kwenda kuangalia Machi live za Laliga" amesema Chuwa.

"Kwa hiyo tunawaomba Watanzania wategemee kupata vitu vizuri katika maeneo mengi lengo ni kuona kwamba kila kundi kwenye jamii ndani nchi yetu inapata kila hitaji lake kutoka katika vyombo vyetu vya habari,"anasema Gloria.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad