JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ZAIDI YA WATU 200,000 WAFIKIWA NA HUDUMA ZA UPIMAJI WA VVU, ZAIDI YA 8,000 WAISHI NA MAAMBUKIZI

Share This

 



Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
IMEELEZWA kuwa kuanzia agosti 2020 hadi kufikia julai 2024 mradi wa USAID huduma za afya kwa Polisi na Magereza umeweza kuwafikia jumla ya watu 223,201 kwa huduma za upimaji wa VVU na kutambua watu waishio na maambukizi ya VVU 8,214 na kuunganishwa na huduma za tiba na matunzo katika vituo vya jirani kulingana na matakwa ya mnufaika wa huduma.

Mkurugenzi wa Huduma za Uangalizi Wizara ya Mambo na Ndani ya Nchi Charles Nsanze ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma alipomuwakilisha Katibu Mkuu wizara ya Mambo ya ndani Kwenye mkutano wa wadau kwa ajili ya kujadili utoaji wa huduma bora za afya katika vituo vya Polisi na Magereza kote nchini.

Nsanze amesema katika kipindi hicho jumla ya wagonjwa wa kifua kikuu 2,797 waligundulika katika vituo vya kutolea huduma na kuanzishiwa matibabu.

"Hii inadhihirisha kazi nzuri inayofanyika katika vituo hivi, naomba nipongeze uongozi wa kikosi cha Jeshi la Polisi na kitengo cha Afya na lishe cha Jeshi la Magereza pamoja na shirika la THPS kwa kusimamia utekelezaji wa afua hizi '

Aidha Nsanze amesema anaamini kwa juhudi hizo za dhati na ushirikiano uliopo itawezekana kufanikisha azma ya serikali ya kuhakikisha kuwa ifikapo 2030 ugonjwa wa UKIMWI na kifua kikuu unadhibitiwa na kuwa sio tishio tena la kuleta maafa Kwa wafungwa, watumishi wa Jeshi la Polisi Magereza, familia zao na jamii inayowazunguka na kuhudumiwa na vituo vya huduma za afya na watanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la THPS George Antony amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali Kupita mradi wa USAID huduma zae afya Kwa Jeshi la Polisi nae Magereza katika kutekeleza afua mbalimbali za VVUna kifua kikuu nchini.

THPS inashirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara za Tanzania Bara na Zanzibar, Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, Wanawake na makundi maalum, Ofisi ya Rais- TAMISEMI na Wizara ya mambo ya Ndani ya nchi katika utoaji wa huduma bora kwa Watanzania wote katika kutoa huduma bora na jumuishi za VVU na Kifua Kikuu

Mradi wa huduma za afya kwa Polisi na Magereza ni mradi wa miaka mitano )Agosti 2020- julai 2025) unaotekelezwa katika wilaya 35 za Tanzania Bara na Zanzibar ili kisaidia upatikanaji wa huduma jumuishi za kinga, tiba na matunzo ya VVU na kifua kikuu katika vituo 64 vya afya vya Polisi na Magereza nchini


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad