JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


RAIS WA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) IKULU ZANZIBAR

Share This

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ashatu Kijaji (kulia kwa Rais) akiwa na ujumbe wake,mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25-9-2024, akiwa na Uongozi wa Wizara yake walipofika kwa ajili ya mazungumzo na kujitambulisha.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) Mhe. Ashatu Kijaji (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25-9-2024, walipofika kwa ajili ya mazungumzo na kujitambulisha.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ashatu Kijaji, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25-9-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ukiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo.Mhe.Ashatu Kijaji (kulia kwa Rais) baada ya kumaliza mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25-9-2024.
(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amezitaka Wizara zenye dhamana ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar kufanyakazi kwa pamoja ili kuzipatia ufumbuzi changamoto za kimazingira na mabadiliko ya tabianchi zinazoibuka maeneo mbalimbali ya nchi.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk. Ashatu Kijaji alieambatana na timu ya watendaji wakuu wa Wizara hiyo, waliofika kwaajili ya kujitambulisha.

Amesema, ni vyema Wizara hizo mbili kuweka mkazo katika kuzipitia Sera, kanuni miongozo, mipango na mikakati ya kudhibiti changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa pamoja ili kubadilishana uzoefu na kuibua utatuzi wa masuala hayo.

Amesema, uvamizi wa majichumvi kwenye maeneo ya kilimo, visima na makaazi ya wananchi, mporomoko wa fukwe za bahari na ukosefu wa mvua na mvua zisizotarajiwa bado ni matatizo yanayoathiri kwa kiasi kikubwa.

Rais Dk. Mwinyi amewataka watendaji wa wizara hizo kutumia makongamano na mikutano ya kimataifa ya kimazingizingira kuziwasilisha changamoto hizo zinaziikabili nchi ili kupata ufadhili na rasilimali za kukabiliana nazo.

Aidha, aliwasisistiza kuwa na mipango shirikishi kuanzia ngazi za chini kwa jamii ili nayo itoe mchango wake.

Pia, Dk. Mwinyi amesema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kuchukua juhudi mbalimbali za kuzuia athari za mazingira zisiendelee kuathiri maisha ya watu.

Akizungumzia masuala ya Muungano, Rais Dk. Mwinyi ameridhia ombi la Waziri Kijaji la kutaka siku tatu kila mwezi kwa watendaji wa Wizara hizo mbili kukutana Zanzibar na kuwa na mikutano na wananchi kutoa maoni yao juu ya changamoto za Muungano.

Kuhusu biashara ya kaboni, (gesi ukaa) Dk. Mwinyi aliwataka watendaji hao kushirikiana kwa pamoja, kujengeana uwezo na kuwatafuta wataalamu kwani biashara hiyo ni mpya ulimwenguni.

Pia, Dk. Mwinyi amesisitiza suala la Uratibu wa shughuli za Muungano kwani sekta zote wanazozisimamia zinahitaji ushirikiano wa karibu ili kuleta ufanisi.

Naye, Waziri Kijaji ameeleza tayari Wizara hiyo imeandaa timu ya wataalamu na imeanza utafiti na kuandika miradi kwa lengo la kuiwasilisha kwa wafadhili ili kupata fedha zitakazoendesha miradi ya kimazingira.

Amebainisha, kuwa uharibifu wa mazingira ni mkubwa hasa katika fukwe unaosababishwa na mmongonyoko na uvamizi wa maji chumvi katika maene ya kilimo, hivyo juhudi za pamoja zinahitajika kukabiliana na hali hiyo.

Waziri Kijaji amefika ikulu kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Julai 03 mwaka huu.

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad