JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MKURUGENZI MKUU TCAA, MSANGI, AKAGUA JENGO JIPYA LA KUONGOZEA NDEGE UWANJA NDEGE SONGEA LINALOTARAJIA KUZINDULIWA NA RAIS DKT. SAMIA LEO SEPTEMBA 23, 2024

Share This

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege wa Mamlaka hiyo, Flora Alphonce, alipokuwa akiwatambulisha Maafisa wa TCAA kabla ya kutoa taarifa fupi ya jengo jipya la kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024. Jengo hilo pamoja na miradi mengine uwanjani hapo inatarajiwa kuzinduliwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 23, 2024. Picha na TCAA.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo, wakati alipokuwa anawasili Uwanja wa Ndege wa Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024, kwa ajili ya kukagua jengo jipya la kuongozea ndege katika uwanja huo, ambalo linatarajiwa kuzinduliwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Septemba 23, 2024 Mkoani humo. Picha na TCAA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kushoto), akisalimiana na Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Songea, Kasmiri Fortunatus, wakati Mkurugenzi Mkuu huyo alipokuwa analikagua jengo jipya la kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024. Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege wa Mamlaka hiyo, Flora Alphonce. Jengo hilo pamoja na miradi mengine uwanjani hapo inatarajiwa kuzinduliwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 23, 2024. Picha na TCAA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege wa Mamlaka hiyo, Flora Alphonce, alipokuwa akitoa taarifa fupi ya jengo jipya la kuongozea ndege, katika uwanja wa ndege Songea, Mkoani Ruvuma, Septemba 22, 2024. Jengo hilo pamoja na miradi mengine katika kiwanja hicho inatarajiwa kuzinduliwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 23, 2024. Picha na TCAA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad