JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


JWTZ WAPEWA MBINU NA MAKOCHA KUTOKA UHOLANZI

Share This

  





Na Khadija Kalili Michuzi Tv 
MKUU  wa Majeshi nchini Jenerali Jacob Mkunda (CDF) kupitia uratibu wa Baraza la Michezo la Majeshi ya Ulinzi Dunia Conseil International du Sports Military imewaleta  wakufunzi na wataalamu kutoa mafunzo kwa  makocha nchini  ikiwa na  lengo la kuwaaendeleza Maafisa  wa Jeshi   na Askari wenye taaluma ya michezo.

 "Mafunzo haya yataimarisha mahusiano mazuri  kati ya Tanzania  na nchi ya Uholanzi (Netherlands)". 

"Dhamira ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ni  kupata waalimu wazuri watakao saidia timu za JWTZ  zinazoshiriki katika  ligi mbalimbali nchini na kimataifa. 

Hayo yamesemwa leo 11,Septemba,
2024  Kocha Rajab Bwamkuu  kutika JWTZ  alipozungumza na Waandishi  wa Habari   kwenye Uwanja wa JKT  Mbweni uliopo Jijini Dar es Salaam.

Kocha Rajab Bwamkuu amezungumza kwa niaba ya wenzake amesema wanatoa  shukran  kwa  Mkuu wa Majeshi CDF Jacob Mkunda  kwa kuona umuhimu wa kuwaleta wakufunzi hao  ambapo mbali na wakufunzi hao kutoka nje pia  Shirikisho la Soka nchini  (TFF) wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali.

 "Waalimu hawa wakigeni wapo mbali kimafunzo  na wanavifaa vya kisasa  hivyo tanatoa ahadi ya kufanya vizuri katika kuhakikisha timu za Majeshi na Taifa zinafanya vizuri" amesema Kocha  Bwamkuu.

Aidha Bwamkuu ametaja majina ya Wakufunzi hao kutoka nchini Uholanzi (Netherlands) ni Rob Van Belkom,
Hans Feensta na Sigi Careera.

"Mafunzo  haya ni ya wiki mbili na ijumaa jioni yatafungwa rasmi hii inatokana na mahusiano mazuri ya Chama Cha Mpira wa miguu Cha majeshi" amesema Bwamkuu .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad