JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


CP KAGANDA ATOA UZOEFU WAKE MASUALA YA POLISI JAMII MAREKANI

Share This

 






 *NI KATIKA NCHI ALIZOHUDUMU KULINDA AMANI, WASHIRIKI WAIPOKEA MBINU HIYO

Na Abel Paul Chicago Marekani.
Ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo kwa askari wa kike na wasikamizi wa sheria duniani yanayoendelea Chicago Nchini Marekani suala la Uzoefu katika Masuala ya Polisi Jamii nalolikatolewa na kamishna wa Polisi Utawala na menejimenti ya rasilimali watu katika maeneo aliyohudum akiwa Mkuu wa Operesheni Abyei Sudan kusini.


CP Suzan Kaganda ametoa uzoefu huo Nchini humo mbele ya maelefu ya waliohudhuria mafunzo hayo ambayo yaliyojusisha Nchi zaidi ya sitini na Nne ambapo ametoa uzoefu wake katika masuala ya Polisi Jamii na namna ambavyo wananchi wanaweza kushiriki kulinda amani ya eneo husika bila ya kuwa na Jeshi la Polisi wala Jeshi lolote katika eneo lenye changamoto ya amani.


Aidha ameongeza kuwa suala la amani ni jambo ambalo linatakiwa kushirikisha Jamii ili amani na utulivu wa eneo husika kuimarika kutokana na ushiriki kamili wa wananchi katika ulinzi wa amani bila ya kuwa na Jeshi la Polisi akiweka wazi kuwa suala la amani ya eneo husika linatakiwa kuanza na Jamii husika.


Sambamba na hilo CP kaganda akasisitiza kuwa suala la Polisi jamii ni njia nzuri katika masuala ya ulinzi wa amani kutoka na tafiti alizozifanya na uzoefu wake akiwa Mkuu wa operesheni za kulinda amani katika eneo Abyei Sudan Kusini.


Mbali na hilo washiriki wengine kutoka Nchini Tanzania wakaeleza namna mafunzo hayo yalivyowaimarisha katika kujiamini kiutendaji na nafasi wanazopewa hudumu huku waki weka wazi kuwa pindi watakaporudi nchini Tanzania watanzania wategemee mabadiliko makubwa kutokana mafunzo hayo.


Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Johari Saidi yeye akaeleza namna mafunzo hayo yalivyowapa mwanga katika mgawanyo wa majukum bila kuathiri familia walizonazo ikiwa ni pamoja na namna Bora ya utunzaji wa afya kwa askari kutokana na unyeti wa majukum makubwa waliyonayovyombo vya ulinzi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad