JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Barrick yatoa kompyuta kwa shule ya wasichana Barbro Johnson kuwawezesha kupata elimu kidigitali

Share This
Mwenyekiti wa taasisi ya Joha Trust na  Mwanzilishi wa shule ya Wasichana ya Barbro Johansson nchini, Profesa Anna Tibaijuka akiongea katika mahafali hayo.

Na Mwandishi Wetu, Michuzi Tv
WANAFUNZI shule ya sekondari ya Wasichana ya Barbro Johansson iliyopo Luguruni jijini Dar es Salaam wametakiwa kuweka bidii kubwa katika masomo yao sambamba na kujiamini na kuwa na nia ya kufuata nyayo za wanawake wanaofanya mambo makubwa ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao za baadaye baada ya kumaliza masomo.

Wito huu umetolewa na Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini (Corporate Communications and Country Liaison Manager), Georgia Mutagahywa, wakati wa mahafali ya 22 ya kidato cha nne shuleni hapo ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Katika mwendelezo wa kuunga mkono kufanikisha elimu kwa watoto wa kike nchini, Barrick imekabidhi msaada wa kompyuta sita za kisasa 15 kwa ajili ya kuimarisha maabara ya kompyuta ya shule hiyo na kuwezesha wanafunzi kupata elimu kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya kidigitali.

Msaada huo umepokelewa kwa furaha na Wanafunzi, wazazi na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Joha Trust inayoendesha shule za Wasichana ya Barbro Johansson nchini, Profesa Anna Tibaijuka, ambaye ameshukuru jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na kampuni ya Barrick na Twiga kwa kuunga mkono na kuboresha sekta ya elimu nchini ambapo ametoa wito kwa wazazi wa Tanzania na taasisi mbalimbali kuwekeza katika elimu ya watoto ili kuwaandaa kuwa wataalamu na kuhimili mabadiliko mbalimbali yanayoendelea kutokea kwa haraka siku hadi siku duniani.

"Safari ya mtoto wa kike ina changamoto nyingi lakini kwa muongozo ufaao wasichana watafanikiwa hata hivyo wasichana wanasisitizwa kujiamini na kuamini ndoto zao na kuthubutu kutafuta ushauri na mwongozo kutoka kwa wale ambao wamefanikiwa kusafiri kwa njia moja". Amesema Profesa Tibaijuka

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa Barrick Georgia Mutagahywa, amesema Barrick itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali na wadau mbalimbali katika kufanikisha vijana wa kitanzania wanapata elimu bora kwa kuwa inaamini elimu bora ni nyenzo kubwa ya kuleta maendeleo katika taifa.

“Msaada tulioutoa kwa shule hii na kwenye shule nyingine mbalimbali nchini ni kwa sababu ya imani yetu kubwa kwamba tukiwezeshwa mtoto wa kike atafanikiwa. Tunaamini katika uwezo wa wasichana na tunatekeleza jukumu letu katika kuwapa nafasi katika elimu bora kwa kuondoa vizuizi vingi kadiri tuwezavyo na kuwapa zana za kuwasaidia kuendelea katika elimu yao,” aliongeza.

Mkuu wa Shule hiyo Jospina Leonidas ameishukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa mafanikio ya shule hiyo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku na kufanikisha ndoto ya kuwa shule bora ya wasichana nchini.
Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini (Corporate Communications and Country Liaison Manager), Georgia Mutagahywa (kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Barbro Johansson ya  jijini Dar es Salaam  ambapo alikuwa mgeni rasmi na kukabidhi kompyuta 15 za kisasa zilizotolewa na Barrick kwa ajili ya kuimarisha maabara ya kompyuta ya shule hiyo. Pembeni kushoto ni uongozi wa shule hiyo ukishangilia


Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Barbro Johansson wakionyesha  kompyuta zilizotolewa na kampuni ya Barrick wakati wa mahafali ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyofanyika hivi karibuni.
Baadhi ya wahitimu katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa shule waliokuwa katika meza kuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad