JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ALAF, URA SACCOS zasaini makubaliano ya kuwezesha ujenzi bora

Share This

  

Meneja Masoko wa Kampuni ya Alaf, Isamba Kasaka (wa pili kushoto),
akibadilishana mkataba na Meneja Mkuu wa Ura Saccos, ACP. Kim
Mwemfula, wakati walipoingia makubaliano ya Saccos hiyo kutumia bidhaa za Alaf jijini Dar es Salaam Jumanne. kushoto ni Mkuu wa Biashara wa Kampuni hiyo, Sateesh Yamsani, na kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Ura Saccos, Christopher Mwambona.
Picha ya pamoja kati ya Kampuni ya Alaf na  Ura Saccos  mara baada ya kusaini makubaliano jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
KAMPUNI ALAF Limited imesaini makubaliano na chama cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia (URA SACCOS), ambapo wanachama watanufaika na suluishi bora za ujenzi zinazozalishwa na ALAF kwa bei ya punguzo maalum.

Hafla ya kutiliana saini ilifanyika katika makao makuu ya ALAF Limited jijini Dar es Salaam kati ya ALAF na URA SACCOS ambayo ina wanachama wapatao 46,000 nchi nzima.

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Meneja Masoko wa ALAF Isamba Kasaka alisema “Tunafurahi kusaini makubaliano haya na URA SACCOS ambayo ni ishara ya mwanzo mpya kwa pande zote mbili kwani utaratibu huo mpya utahakikisha wanachama wanapata suluishi mbalimbali za ujenzi zenye ubora wa hali ya juu, kwa bei nafuu.”

"Kufuatia makubaliano haya wanachama watahitajika kuagiza kupitia SACCOS yao ili kuweza kupata punguzo maalum" alisema mkuu huyo na kuongeza. Kwamba SACCOS itawajibika kufanya mchakato wa malipo kwa niaba ya wanachama wake.

Aidha alibainisha kwamba Kampuni ya ALAF ilikubali kuingia katika makubaliano haya ili kuunga mkono jeshi la polisi ambalo linawajibu wa kulinda usalama wa raia.

"Mnapotekeleza wajibu wenu wa kulinda usalama wetu, ni muhimu mpate faraja kwamba nyumbani kuna amani kwa sababu ya nyumba zimejengwa kwa ubora," alisema.

Alisema milango ya ALAF iko wazi kwa SACCOS, vyama au mashirika mengine yanayotaka kuingia makubaliano ya aina hii ili kuhakikisha wanapata suluhisho bora na thamani ya fedha zao.

Kwa upande wake, kamishina msaidizi wa jeshi la polisi na meneja mkuu wa URA SACCOS Acp Kim Onai Mwemfula aliishukuru Kampuni ya ALAF kwa kuwapa fursa ya pekee ambayo itawarahisishia wanachama wao kujenga nyumba bora na za kisasa kwa gharama nafuu.

"Tuna wanachama wapatao 46,000 na moja ya maono yetu ni kuona sisi sote tunajenga nyumba nzuri kwa gharama nafuu. Utaratibu huu mpya na ALAF utarahisisha hili na kuhakikisha wanachama wetu wanapata suluisho bora za ujenzi kutoka ALAF,” alisema.

Alitoa wito kwa wanachama kutumia fursa ya makubaliano hayo na kuagiza kwa wakati ili kuhakikisha vifaa vyao wanaletwa kwa haraka.

Kampuni ya ALAF inaongoza nchini Tanzania kwa kutengeneza vifaa bora vya mapaa. Ilianzishwa mwaka 1960, na imekuwa daima, na inaendelea kuwa, mdau muhimu katika maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini. ALAF si tu inazalisha vifaa vya chuma vya kuezekea, bali pia koili za metali zitumikazo katika shughuli uezekaji wa nyumba. ALAF pia hutengeneza mabomba ya metali na ya aina nyingine kwa matumizi mbalimbali.

www.alaf.co.tz

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad