JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WAFANYABIASHARA WA TANZANIA WAASWA KUUZA BIDHAA ZA VYAKULA NCHINI CHINA

Share This

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa kongamano lililokutanisha wawekezaji kutoka China na Tanzania. Kongamano hilo limefanyika leo Agosti 22 jijini Dar es Salaam.

upande wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida akizungumza wakati wa kongamano la Ushirikiano kati Tanzania na China lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 22, 2024.
Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian akizungumza wakati wa kongamano la Ushirikiano kati Tanzania na China lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 22, 2024.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
KATIKA kuadhimisha ya miaka 60 ya  mahusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya watu wa China watanzania wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo China hasa katika kuuza bidhaa za vyakula katika nchi ya China.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo wakati wa Kongamano lililolenga kukuza ushirikiano endelevu wa pamoja wa siku zijazo katika nchi zote mbili. Kongamano hilo limefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 22, 2024.

Prof Kitila amesema kuwa wafanyabiashara wa Tanzania wanatakiwa kupeleka bidhaa mbalimbali hasa za kilimo nchi ya China ambapo China inaweza wa kuzichukua zote na zisitoshe kulingana na uwingi wao. 

"Bidhaa ambazo zinahitajika nchini China ni pamoja na Korosho, Asali, Chai na Kahawa, Mihogo pamoja na Viazi vitamu na kwenye uchumi wa Buluu wanahitaji zaidi Samaki, Mabondo." Amesema Prof. Kitila

Amesema mwelekeo, msimamo na msukumo mkubwa kwa Watanzania kwa sasa nikuona wanaongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini China. 

"Ushirikiano wetu umefungua fursa na kazi kubwa kwa Wafanyabiashara Watanzania  kuongeza bidii kwa sababu bidhaa nyingi zinahitajika kwa kiwango ambacho hazitatosha nchi China"

Amesema kitu ambacho ni tofauti kati ya Tanzania na China, Wachina wanauza zaidi bidhaa zao hapa nchini kuliko watanzania kuuza bidhaa nchini China, amesea tunahitaji kuweka mizani sawa ya uuzaji wa biashara katika nchi hizi mbili kwa ukaribu zaidi. 

"Wachina ndio wanaoongoza katika uuzaji wa bidhaa hapa nchini ukilinganisha na nchi nyingine ambapo zamani walikuwa ni wamarekani, Kenya."

 Kwa upande wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida amesema kuwa kuanzia Januari 2021 hadi Juni 2024, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kilisajili miradi 1,360 inayotarajiwa kuajiri 155,596 na kuwekeza mitaji yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 11,586 huku sekta tano bora zikiwa ni viwanda, ujenzi wa biashara, kilimo, usafirishaji na huduma.

 "China ni chanzo kikuu cha Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni nchini Tanzania."

Pia amewashukuru  Serikali ya China kuanzisha mpango Barabara, unaojulikana nchini China kama mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja." Mkakati wa kimataifa wa maendeleo ya miundombinu uliopitishwa na Serikali ya China mwaka 2013 kuwekeza katika nchi zaidi ya 150 na Tanzania ikiwemo."

Kwa upande wa Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian amesema kuwa masoko ya China yanaagiza Asali tani zaidi ya milioni 32 kwa mwaka huku jumla ya uzalishaji wa asali nchini ni tani 32000 amesema hiyo ni sehemu ndogo ya mahitaji ya Asali nchini China.

Wakizungumza katika majadiliano ya awamu ya kwanza wamependekeza kuwepo kwa fedha za China (Yuan) na Shilingi ya Tanzania wakati wa biashara ya nchi hizi kwa sababu haina umuhimu wa kutumika dola kwani hakuna biashara kati ya wanaotumia dola kati ya nchi hizi.

Pia katika majadiliano hayo wamependekea kujengwa kwa Daraja kati ya Tanzania bara na Zanzibar ili kurahisisha hali ya usafiri katika maeneo hayo.




Baadhi ya Wadau wa Uwekezaji wakiwa katika kongamano lililofanyika leo Agosti 22, 2024 jijini Dar es Salaam.

Picha za pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad