KAMPUNI ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Huawei Tanzania wamezindua darasa ya kidigitali inayoitwaa digi truck, ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua kama mgeni rasmi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo leo Agosti 24, 2024 amesema serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili iweze kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi kama inavyoelekezwa katika Dira ya Taifa ya 2025, Sera ya Maendeleo ya TEHAMA ya mwaka 2016 na Ilani ya CCM 2020-2025.
Amesema kuwa, Serikali inahamasisha matumizi ya TEHAMA ili kuwezesha wananchi hususani vijana na kizazi kijacho kushindana katika uchumi wa dunia.
"Kwa kuimarisha elimu ya TEHAMA, tunajenga jamii yenye ujuzi wa kutumia teknolojia kwa ufanisi, kubuni suluhisho za ubunifu, na kuchangia katika uchumi wa kidijitali. Hii itasaidia katika kuhakikisha kwamba maendeleo ya kidijitali yanakutanisha kila mmoja, bila kujali hali ya kiuchumi." Amesema Dkt. Biteko.
Ameongeza kuwa, Serikali inayoongozwa na Rais Samia itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba wawekezaji wanakuwa msaada katika kubadilisha hali maisha ya watu kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo TEHAMA huku pia wawekezaji hao wakinufaika na uwekezaji wao.
Dkt. Biteko amesema uchumi wa kidijitali ni muhimu katika kuleta maendeleo kwa kuongeza ufanisi katika uzalishaji na na kuleta fursa na mapato ya ziada kwa wananchi.
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa amewapongeza Huawei na Vodacom kwa kuja na teknolojia ya Digi Truck ambayo inakwenda kuwa msaada kwa vijana wengi nchini ambayo itafika kila sehemu ili vijana wengi wajifunze.
Teknolojia hiyo iliyozinduliwa leo kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania na Huawei itawezesha wananchi kupata elimu na ujuzi wa TEHAMA.
Nae Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Philip Besiimire amesema Mpango huo unalenga kuwapatia Watanzania ujuzi wa msingi wa kidijitali na kuwaboreshea ujuzi na maarifa, ukilenga wanafunzi zaidi ya 5,500, wanawake, na vijana katika mikoa 10 kila mwaka kwa kipindi cha miaka 3 ijayo.
Aidha amesema kuwa Programu hiyo itatoa uzoefu wa kujifunza wa kubadilisha maisha kupitia vipindi viwili maalum, ambapo kuna Programu ya siku 6 katika shule za sekondari kwa vijana wa umri wa miaka 16 hadi 19, na
Programu ya wiki 2 kwa vijana waliojiajiri na wanawake wajasiriamali wenye umri wa miaka 20 na kuendelea.
Amesema Darasa hilo la kidijitali linalotembea linaonesha kujitolea kwao kuwawezesha Watanzania kupata ujuzi muhimu wa kidijitali, hususani kwa maeneo na watu walio na upungufu wa fursa.
"Kupitia programu maalum kwa shule za sekondari, vijana waliojiajiri, na wanawake wajasiriamali, DigiTruck inalenga kuwawezesha Watanzania na nyenzo wanazohitaji ili kufanikiwa katika ulimwengu unaozidi kuwa wa kidijitali". Amesema
Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (wa nne kulia) akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa Wote (DigiTruck) tukio lililofanyika leo Agosti 24,2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa Wote (DigiTruck) tukio uliofanyika leo Agosti 24,2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa Wote (DigiTruck) tukio uliofanyika leo Agosti 24,2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Philip Besiimire akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa Wote (DigiTruck) tukio uliofanyika leo Agosti 24,2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huawei, Damon zhang akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa Wote (DigiTruck) tukio uliofanyika leo Agosti 24,2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akimfurahia Mwanafunzi wa Darasa la sita, Jasmine Ali kutoka Shule ya Msingi Oysterbay baada ya kumpisha Mimbari kwa ajili ya kuwasilisha shukrani kwa nimba ya Wanafunzi walioshuhudia Uzinduzi wa Mpango wa Ujuzi wa kidigitali kwa wote (DigiTruck), Tarehe 24, Agosti 2024, Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment