JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Tanzania yajiweka mahala pazuri katika utekelezaji wa mkataba IOMOU

Share This

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Haji Makame akizungumza wakati akifunga Mkutano wa 27 wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi  (IOMOU) wenye lengo la kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya ukaguzi meli zinazoingia katika bandari za nchi wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Usalama  wa Usafiri na  Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi Stella Katondo akitoa maelezo kuhusiana na Mikakati ya usimamizi  wakati kufunga  Mkutano wa 27 wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi  (IOMOU) wenye lengo la kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya ukaguzi meli zinazoingia katika bandari za nchi wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Usalama  wa Usafiri na  Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi Stella Katondo akitoa maelezo kuhusiana na Mikakati ya usimamizi  wakati kufunga  Mkutano wa 27 wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi  (IOMOU) wenye lengo la kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya ukaguzi meli zinazoingia katika bandari za nchi wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Matukio ya picha wakati wa ufungaji wa Mkutano wa 27 wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi  (IOMOU) wenye lengo la kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya ukaguzi meli zinazoingia katika bandari za nchi wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam.



*TASAC yaweka mikakati katika usimamizi utekelezaji wa mkataba kwenda katika uchumi wa Bluu

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
IMEELEZWA kuwa Tanzania imeweza kutekeleza hati ya makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi (IOMOU) katika kufanya ukaguzi wa Meli za Kigeni na kuwa mfano wa kuigwa.

Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu ,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Haji Makame wakati akifunga mkutano wa 27 wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi (IOMOU) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema tangu kuingia kwa makubaliano hayo Tanzania imefikisha miaka 25 na kuwa na matokeo chanya kutokana jitihada za Serikali kutoa mafunzo mbalimbali ya wakaguzi wa Meli ndani na nje ya nchi na kuweza kukagua vyombo vya majini 300.

Amesema kuna changamoto huwa zinakuwepo lakini huwatuwezi kuziona kutokana na umoja huo wa makabaliano Kuna kuwa Kuna waguzi ambao wakitoa ripoti na wanazileta na Serikali kufanyia kazi.

Makame amesema ziko Jumhiya Sita ambazo ziko nje ya Bahari ya Hindi ambao wamekuja na kuona mabadiliko kuhusiana na Utekelezaji wa makubaliano kwa nchi wanachama.

Amesema kuwa kuna utaratibu wa kubadilishana taarifa za vyombo ambavyo vinatoka Tanzania vikionekana katika nchi wanachama wanatoa taarifa kuhusiana na masuala ya ukaguzi.

Aidha amesema miaka 25 nchi imekuwa katika mkakati wa kuhakikisha vyombo vya usafiri majini vinakuwa salama.

Amesema kadri nchi inavyofanya vizuri ndio inafanya kuwepo matokeo mazuri kutokana na vigezo vilivyowekwa na nchi wanachama.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Nahson Sigalla amesema ni mkutano maalum umeshirikisha nchi wananchama Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli za Kigeni katika ukanda wa Bahari ya Hindi ukiwa lengo ya kuimarisha usalama katika vyombo.

Amesema kuimarisha usalama ni kulinda mazingira na matokeo yake kupata maendeleo endelevu yanayofanya kukia.

Amesema Tanzania imekuwa mfano katika ukaguzi wa Meli kutokana mafunzo kwa wakaguzi kutokana na Meli zilizopo ni za kisasa.

Sigalla amesema wamekubaliana Kila nchi wanachama kufanya ukaguzi wa Meli za Kigeni angalau asilimia 10 ili kuweza kuwa na usalama wa kufanya nchi wananchama ziendelee kupata maendeleo.

Amesema kuwa katika kufanya ukaguzi na kulinda mazungira ndio nguzo katika kwenda katika uchumi wa Bluu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad