JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


"KAMA JINA LA FILBERT BAYI LINAWAKWAZA LIONDOLEWE" BAYI

Share This

 






Na Khadija Kalili Michuzi Tv
"Inafika wakati natamani kusema kama tatizo ni hili jina langu ndiyo linasababisha hii barabara kutotengenezwa basi waliondoe huenda kuna watu linawakwaza lakini wakumbuke hii siyo njia yangu binafsi huku kuna wanafunzi ambao wanapita kutoka Shule tofauti, wanajeshi na wananchi wa kawaida wote wanatumia njia hii."

Hayo yamesemwa Agosti 24, 2024 na Meja Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania ambaye pia alikuwa mwanariadha aliyeng'ara katika medani ya mchezo wa riadha Olympic mwaka 1974 Filbert Bayi wakati wa mahafali ya shule ya Filberth Bayi amesema kuwa Shule yake yakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya barabara.

"Tangu nianzishe Shule hii ya Filbert Bayi changamoto kubwa tunayokumbana nayo ni barabara kupitika kwa taabu."

Meja Mstaafu Bayi katika mahafali ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Filbert Bayi iliyopo Kimara na Shule ya Msingi na Sekondari Mkuza wanaosoma Shule ya Filbert Bayi iliyopo Mkuza Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

"Nimesha fanya jitihada binafsi miaka yote tangu Shule hii ilipoanza 2006 hadi sasa ikiwa ni pamoja na kuweka mawe kwenye barabara kuchonga kwa kupitisha greda lakini sasa hivi nimechoka sababu hii siyo njia yangu binafsi." Amesema Bayi

Bayi ameongeza kwa kusema kuwa mbona zipo barabara nyingi za watu mashuhuri nyingi zinafanyiwa matengenezo kwanini hii yenye jina la Filbert Bayi haithaminiwi?amehoji Mwanariadha aliyevunja rekodi ya Olympic na Meja Mstaafu wa JWTZ.

Bayi ameongeza kwa kusema kuwa Kamati ya Bunge ambao walitembelea Shuleni hapo hivi karibuni walikwama kwenye barabara hiyo na wakampigia simu Meneja TARURA, anashukuru wananchi wamepaza sauti zao TARURA wamemwaga kifusi na kusisitiza wajitahidi kufanya matengenezo katika barabara hivyo kwani utabiri wa hali ya hewa wametoa tahadhari kuna mvua zitanyesha hivi karibuni.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Kaimu Mkurugenzi Fedha na Utawala Chuo Cha Diplomasia Jacob Nduye amewaasa wanafunzi waliohitimu kuishi kwa kumtanguliza Mungu, kuwa na heshima na utii na kuzidisha juhudi ya msingi bora waliopatiwa shuleni hapo sambamba na kuendeleza sifa njema ya Shule hiyo kwani kuna rekodi ya wanafunzi waliohitimu shuleni hapo wengi wamepata nafasi nzuri katika ngazi za serikali na sekta mbalimbali.

Bayi anashikilia rekodi ya kukimbia KM1500 katika michezo ya Jumuia ya Madola ya mwaka 1974 aliposhinda Medali ya dhahabu.

Aidha Filbert Bayi ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC) na hivi karibuni Agosti 6 mwaka huu amepewa heshima ya kuwa miongoni mwa wanariadha nyota waliovunja rekodi za dunia. ambapo Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani Lord Sebastian Coe ndiyo aliandaa hafla hiyo na Bayi amejumuishwa rasmi kwenye jumba la Makumbusho la wanariadha nguli Duniani iliyopo Jijini Paris nchini Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad