JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


DHL kufikia utoaji sifuri wa kaboni ifikapo 2050

Share This

Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika wa DHL Express Bi Fatima Sullivan (katikati) akijadiliana jambo na Meneja wa DHL nchini Bw Humphrey Pule (kulia) wakati wa mkutano maalumu kati ya kampuni hiyo na maofisa watendaji wa makampuni mbalimbali Jijini Dar es Salaam Jumatano. Kushoto ni Meneja Biashara Bw Thierry Ayishashe.
Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika wa DHL Express Bi Fatima Sullivan (katikati) akijadiliana jambo na Meneja wa DHL nchini Bw Humphrey Pule (kulia) wakati wa mkutano maalumu kati ya kampuni hiyo na maofisa watendaji wa makampuni mbalimbali Jijini Dar es Salaam Jumatano. Kushoto ni Meneja Biashara Bw Thierry Ayishashe.

DHL Express, ambayo ndiyo kampuni kubwa zaidi ya usafirishaji duniani, imeelezea kujitolea kwake kufikia utoaji wa kaboni sifuri ifikapo mwaka 2050 katika jitihada zake za kufanya kazi katika mazingira yaliyo safi zaidi.

Akizungumza wakati wa kifungua kinywa kwenye meza ya mazungumzo ya maofisa watendaji wakuu yaliyoandaliwa na DHL, Mkurugenzi wa Kanda wa Nchi za Kusini na Afrika Mashariki, Bi Fatima Sullivan, miongoni mwa mambo mengine, alisema hilo ni miongoni mwa vipaumbele vya kampuni ya DHL.

"Ndege zetu zinafanya kazi duniani kote kusafirisha mizigo na hutoa kaboni nyingi. Tunafanya kazi ili kuhakikisha kuwa utoaji wa kaboni unafikia mwisho (sifuri) ifikapo mwaka 2050, "aliwaambia maofisa watendaji wakuu kutoka sekta mbalimbali.

Aidha, alisema kwamba kuna utafiti na majaribio ya aina mbalimbali juu ya ndege za umeme ambazo hazitoi kaboni. "Ni utafiti wa kina ambao utachukua muda kwa sababu sisi sote tunajua sekta ya usafiri wa anga ni changamani na nyeti.”

Bi Sullivan pia alisisitiza kujitolea kwa DHL kwa ajenda ya kijani ambayo kupitia kwayo kampuni yake itawashirikisha wenyeji kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa. “Tunapanga kutekeleza miradi mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira ambayo itatusaidia kutoa huduma bora zaidi,” alisema.

Kuhusu mazingira ya biashara nchini Tanzania, Bi Sullivan aliwaambia maofisa watendaji wakuu kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi tano zinazokua kwa kasi kubwa Afrika na mdau muhimu katika kanda, hivyo ni nchi ya kimkakati wa kibiashara.

Alionyesha umuhimu wa biashara ndogo na za kati na nafasi yake katika biashara ya DHL, hivyo wataendelea kuziendeleza kwa kuzijengea uwezo zaidi na kuhakikisha zinarasimishwa na zinaweza kufanywa kwa urahisi ndani na nje Tanzania.

"Tuna bidhaa inayojulikana kama SME 360, ambayo tutahakikisha biashara ndogo na za kati na ambazo mingoni mwake kuna za kifedha na taasisi za biashara zinaendeshwa vizuri,” alisema.

Naye Meneja wa DHL nchini, Bw Humphrey Pule, alisema walifurahi sana kuwa mwenyeji wa meza ya mazungumzo ya wakati wa kifungua kinywa kwani imewapa DHL na wadau wao maarifa mengi kuhusu mazingira ya biashara na jinsi gani kwa pamoja wanaweza kutatua baadhi ya changamoto zinazoathiri biashara nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na miundombinu na taratibu za udhibiti.

"Tunatazamia kuwa mwenyeji wa mikutano mingi zaidi kwa siku zijazo kwani ni muhimu kwa biashara,” alisema.

Tukio hili liliwaleta pamoja maofisa watendaji wakuu na baadhi ya wabia wa DHL ambao wanafanya kazi ndani na nje ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad