-Azitolea maelekezo,
-Amshukuru Waziri Mkuu kumuagiza Naibu Waziri haraka masuala ya NIDA Kagera
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amemuelekeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki kuifanyia kazi na kupata ufumbuzi wa changamoto ya wanyama waharibifu wanaovamia makazi ya watu, kuharibu mazao na kutishia uhai wa binadamu, Wilaya ya Karagwe.
Vile vile, Katibu Mkuu Balozi Dkt. Nchimbi amezielekeza mamlaka husika mkoani Kagera, kwa kushirikiana na wizara za kisekta husika, kushughulikia na kumaliza tatizo la matumizi ya ardhi, mipaka kati ya wananchi na Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO, wilayani Karagwe.
Balozi Nchimbi ametoa maelekezo hayo alipokua akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kituco cha Mabasi cha Kayanga, wilayani Karagwe, mkoani Kagera, akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita mkoani humo, ambapo miongoni mwa kero za wananchi wa jimbo alizotaarifiwa, ni pamoja na uvamizi wa wanyama hao wakali katika vijiji vya Kata ya Kihanga (Kihanga, Kibwela na Mshabaiguru), ambako Tembo wanavamia mashamba ya wakulima, kuharibu mazao na kuhatarisha maisha wa wananchi katika maeneo husika.
Aidha, alitaarifiwa kuhusu kuwepo mgogoro wa ardhi Kata ya Rugera, kati ya wananchi na Shirika la NARCO katika Kijiji cha Omukakajinja, ambapo alitoa maelekezo, kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kuziagiza mamlaka zinazohusika, zikiwemo za kisekta, kufanyia kazi masuala hayo na kumpatia taarifa za kumalizika kwa migogoro hiyo.
Balozi Dokta Nchimbi ametaka changamoto hiyo ishughulikiwe haraka ikiwemo kutafuta namna ya kudhibiti wanyama waharibifu hasa Tembo lakini pia suala la mipaka ili ijulikane.
Katika hatua nyingine Balozi Dokta Nchimbi amemshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kwa kuusikia wito wa suala la Vitambulisho vya NIDA, na kumuagiza Naibu Waziri wa Mambo ya ndani afike Kagera kuungana na Katibu Mkuu kuwa sehemu ya msafara wa ziara hiyo, ili atolee ufafanuzi na kujibu malalamiko ya wananchi kuhusu jambo hilo.
Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Nchimbi yuko ziara ya siku sita, Mkoa wa Kagera, akiwa ameambatana na Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) - Oganaizesheni, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo na Ndugu Rabia Abdalla Hamid, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Post Top Ad
CHANGAMOTO YA ARDHI NA TEMBO KARAGWE, ZATUA KWA NCHIMBI
Share This
Tags
# SIASA
Share This
Jiachie Blog
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
Newer Article
MAYA’S TREASURE SLOTI YA USHINDI WA 95%
Older Article
NCHIMBI AWAITA MAMBO YA NDANI ZIARA YAKE KUJIBU MASUALA YA NIDA
MBOWE AWAAGIZA VIONGOZI WAPYA CHADEMA KUUNDA KAMATI YA KUPONYA MAKOVU YA KAMPENI
Ahmad MichuziJan 22, 2025MBOWE ADONDOKEA PUA NAFASI YA UWENYEKITI CHADEMA, LISSU ACHUKUA NAFASI
Ahmad MichuziJan 22, 2025RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ANYOOSHA NJIA URAIS WA DK.SAMIA NA DK.MWINYI 2025
Ahmad MichuziJan 19, 2025
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment