JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


YAJUE KUHUSU FAINALI YA SPAIN VS ENGLAND

Share This

 

MICHUANO ya EURO 2024 inaendelea ukingoni ambapo Jumapili hii majira ya saa nne usiku ambapo mpaka kufikia hapa tumeshuhudia mechi kali sana huku timu mbalimbali zikishindana vikali kuwania taji hili. Nani ni nani Jumapili hii?

Waswahili husema kuwa kila lenya mwanzo lina mwisho, basi ndivyo ambavyo ilivyo kwani siku ya Jumapili kutakuwa na fainali nzito kati ya Spain dhidi ya England katika dimba la Olympiastadion huku Meridianbet wakimpa nafasi ya kutwaa taji hili kwa ODDS 2.45 kwa 3.52.

Uingereza chini ya kocha mkuu Gareth Southgate hii inaenda kuwa ni fainali yao ya pili mfululizo kwenye michuano ya EURO baada ya Urusi kufanya hivyo mwaka 1960 na 1964, Ujerumani 1972, 1976, 1976, 1980, 1992 na 1996 na Spain kwenda fainali 2008 na 2012.

Mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane ni mchezaji wa tatu kufunga kwenye nusu fainali za EURO huku mara mwisho kufanywa hivyo ilikuwa ni kwa wachezaji wa Urusi Viktor Ponedelnik na Valentin Ivanov mwaka 1960 na 1964.

Fainali ya EURO 2024 kupigwa Jumapili hivyo jiandae kupiga pesa sasa ukiwa na mabingwa wa ODDS KUBWA Tanzania Meridianbet? Cheza pia michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.

Pia Uingereza imepoteza mechi 1 pekee tu kati ya 20 zilizopita za mashindano huku wakishinda mechi 12 na kutoa sare 7, huku hii ikiwa ni mechi ya tatu kukutana na Spain kwenye EURO.

Mwaka 1980 timu hizi zilikutana hatua ya makundi huko Naples ambapo Uingereza walishinda 2-1 dhidi ya Spain ingawa wote hawafika mbali walitoka kwenye mashindano hayo. Mwaka 1996 walikutana hatua ya 16 bora Uingereza alishinda kwa penati baada ya kwenda dakika zote bila kufungana. Beti sasa.

Pia walishawahi kukutana kwenye kombe la Dunia 1950 na Spain wakaibuka na ushindi, huku hivi karibuni walipokutana Uingereza alishinda 3-2 kwenye mashindano ya ligi ya mataifa huko Seville.

Wakati Uingereza wakionekana kupewa njia nyepesi kufika fainali za EURO 2024, Spain wameonekana wakipita njia ngumu mpaka kufika hapa walipo.

Hispania chini ya kocha mkuu Luis de la Fuente wamemfunga Croatia ambaye alifika nusu fainali kombe la Dunia 2018, wakamfunga bingwa mtetezi wa EURO Italia. Robo fainali wamemfunga mwenyeji wa michuano hii Ujerumani ambayo ilikuwa ni ya pili kusifiwa kwa ubora.

Hatua ya nusu fainali wamemfunga bingwa wa Kombe la Dunia 2018 na wamanafainali wa kombe la Dunia 2022 Ufaransa.

Lakini si hivyo tu, Spain wameshinda mechi zote bila hata kupata bao la penati na kukiwa hakuna timu ambayo imeweza kufanya hivyo. Pia ndio inaongoza kwa ufungaji bora wa michuano hii wakiwa na mabao 13.

Spain pia wana historia kwenye EURO wakishinda taji hili mara tatu 1964, 2008 na 2012, huku ikishinda inakuwa timu ya kwanza kuchukua kombe hili mara 4.

Hispania wana nyota wa mashindano Lamine Yamal ambaye ndio mchezaji mdogo wa mashindano haya. Mchezaji huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 16 amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea kwenye michuano ya Ulaya alipoanza mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Croatia.

Katika nusu fainali juhudi zake za kutwaa tuzo ya mfungaji bora zilimfanya kuwa mfungaji bora mwenye umri mdogo zaidi katika michuano ya Euro akivunja rekodi ya Pele ya Kombe la Dunia. Pia amevunja rekodi ya Pele ya mchezaji mdogo zaidi katika nusu fainali katika mashindano yote mawili.

Sio tu kwamba amekuwa akicheza na kufunga moja ya mabao ya mashindano lakini kitakwimu amekuwa mmoja wa wachezaji bora pia, akiwa na asisti tatu na nafasi 13 alizotengeneza.

Kikosi cha Luis de la Fuente pia kina kiongozi wa sasa katika mbio za Kiatu cha Dhahabu, kiungo wa Leipzig Dani Olmo. Licha ya kuanza michezo miwili pekee amefunga mabao matatu sawa na wachezaji wengine wanne lakini pia ametoa pasi mbili za mabao.

Mwingine anayewania tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo ni kiungo mkabaji wa Manchester City ya Uhispania Rodri.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye alizaliwa siku ambayo Uingereza iliiondoa Uhispania kwenye Euro 1996, amepoteza mchezo mmoja tu kati ya 79 alizocheza kwa klabu na nchi.

Je nani kuchukua taji la EURO 2024?. Suka jamvi lako na Meridianbet ambao tayari wameshakuwekea ODDS za maana na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad