JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Watumishi Housing Kujenga Nyumba 101 za kisasa Mikocheni

Share This
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) Dkt. Fred Msemwa (kulia) wakipongezana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group nchini Tanzania, Li Manchao leo Julai 30, 2024, Dar es Salaam baada ya kutia saini ya makubaliano ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
SHARE




Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) Dkt. Fred Msemwa (kulia) wakipongezana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group nchini Tanzania Bw. Li Manchao leo Julai 29, 2024, Dar es Salaam baada ya kutia saini ya makubaliano ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) Dkt. Fred Msemwa akizungumza jambo leo Julai 29, 2024 Dar es Salaam katika hafla fupi ya utiaji saini na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group kwa ajili ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ushauri na Ubunifu – WHI Arch. Sephania Solomon akizungumza jambo leo Julai 29, 2024, Dar es Salaam katika hafla fupi ya utiaji saini na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group kwa ajili ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
Meneja wa Biashara Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group Bw. Meng Lingyang akizungumza jambo leo Julai 29, 2024, Dar es Salaam katika hafla fupi ya utiaji saini na Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) kwa ajili ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) Mwanasheria Joel Maeda (katikati) akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group nchini Tanzania Bw. Li Manchao katika hafla fupi ya utiaji saini na Mkandarasi wa Kampuni hiyo kwa ajili ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) Dkt. Fred Msemwa (kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group nchini Tanzania Bw. Li Manchao wakiwa katika picha ya pamoja leo Julai 29, 2024, Dar es Salaam wakati wakitia saini ya makubaliano ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
  


Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
TAASISI ya Nyumba ya Watumishi Housing Investment(WHI) hivi karibuni inatarajia kuanza kutekeleza mradi wa nyumba 101 katika eneo la Mikocheni Regent Estate jijini Dar es Salaam wenye thamani ya Shilingi Bilioni 18.6.


Ujenzi wa jengo hilo la gorofa 12 ni sehemu ya nyumba 218 zitakazojengwa katika mikoa ya Dodoma, Lindi, Mtwara, Singida Pwani na Ruvuma ikiwa ni sehemu ya utekelzaji wa mpango wa makazi kwa Watumishi wa Umma.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 30,2024 wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa nyumba hizo na mkandarasi Shandong Hi-Speed Group kutoka China Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Fred Msemwa amesema ujenzi wa nyumba hizo utakamilika katika kipindi cha 0miezi 18.


"Nyumba hizi zitauzwa kwa utaratibu maalamu wa unafuu kwa watumishi wa umma ambapo bei ya nyumba ya chumba kimoja yenye sebule, chumba cha kulala, Choo, stop, kiko, balcony itaanzia sh. Milioni 99 na bei ya nyumba ya vyumba vitatu vya kulala itaanzia sh. Milioni 234". Amesema Dkt. Msemwa.


Dkt. Msemwa amesema bei za nyumba hizo ni nafuu kwa asilimia 10 hadi 40 hasa ukilinganisha na nyumba zingine kama hizo eneo la Mikocheni.


Amesema, teyari uuzwaji wa nyumba hizo umekwishaanza na ni matarajio yao kuwa watapata muitikio mkubwa kutoka kwa walengwa kwani kila mnunuzi atamilikishwa nyumba atakayonunua.


Tunatarajia muitikio utakuwa mkubwa kutoka kwa walengwa kwani mradi huu unalenga kuwapa Watumishi wa umma fursa bora za umiliki wa makazi yenye thamani bora.


Amesema kuwa katika kufanisha ujenzi wa mradi huo watashirikiana na kampuni ya kizalendo katika kusimamia ili kuhakikisha wanapata uzoefu kutoka kampuni ya kichina.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ushauri na Ubunifu WHI Arch. Sephania Solomon, amesema kuwa mradi huo utajengwa kisasa ambapo utakuwa wa ghorofa 12 pamoja na mazingira unaoendana na masisha ya sasa.


Amesema utakuwa na miundombinu ya kisasa ikiwemo mifumo ya kidigitali ili kuhakikisha watumishi wa umma wanaishi katika mazingira rafiki.


Kwa upande wa Meneja wa Biashara Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group Meng Lingyang , amesema kuwa watahakikisha wanatekeleza mradi kwa ufanisi na wataikabidhi kwaa wakati kadiri ya mkataba walioingia


Watumishi Housing Investnent ni taasisi ya umma ambayo inafanya kazi chini ya Ofisi ya Rais UTUMISHI yenye jukumu la kuendeleza milki na usimamizi wa uwekezaji kupitia uanzishaji na usimamizi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja, WHI kwa sasa inasimamia mifuko miwili ambayo Mfuko wa Nyumba Pamoja na mfuko wa Faida Fund. Mpaka sasa tayari wamejenga nyumba 1,003 katika mikoa 19 nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad