JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WAFANYABIASHARA WA KIKOREA WAADHIMISHA SIKU YA BIASHARA YA KOREA WAMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA

Share This

 

Mkurugenzi wa Tantrade, Latifa Khamis akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Biashara ya Korea katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maalufu kama Saba saba.yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mtafiti Mwandamizi Na Mshauri wa Masuala ya Siasa na Uchumi kutoka Ubalozi wa Korea hapa nchini, Hyunseok Jeon akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa Maadhimisho ya siku ya Biashara ya Korea katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maalufu kama Saba saba yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Na Maendeleo ya Viwanda, Fatma Mabrouk Khamis akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Biashara ya Korea katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maalufu kama Saba saba yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.

KATIKA kusheherekea siku Siku ya Korea ya Biashara Wafanyabishara wa Kikorea waadhimisha siku hiyo katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’ huku wakijafiliana namna ya kuendelea kushirikiana na Tanzania katika Uwekezaji.

Akizungumza leo Julai 06, 2024 wakati wa kusheherekea siku hiyo ya Kibiashara, Mkurugenzi wa Tantrade, Latifa Khamis amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake na kuwezesha biashara kufunguka baada ya Tanzania kuonekana kuwa sehemu bora ya kuwekeza.

Amesema Uongozi wa Rais ndio chanzo ambacho kimepelekea wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni kumiminika hapa nchini kuja kuwekeza.

"Ushirikiano wa kibiashara katika Tanzania na Korea  unapelekea maadhimisho haya ya Kibiashara ya Korea kufanyika kwenye viwanja hivi na kuhudhuriuwa na wadau mbalimbali."

Maadhimisho hayo ya siku yaKibiashara ya Korea yameadhimishwa kwa Kuonesha bidhaa mbalimbali pamoja na utamaduni wao.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Na Maendeleo ya Viwanda, Fatma Mabrouk Khamis aliyemuwakilisha waziri wake, Omary Said Shaaban ameipongeza hafla hiyo iliyowakutanisha wafanyabiashara wa Korea na Tanzania na kubadilishana ujuzi.

Fatma ameyasifu maonesho yaliyofanywa kwenye hafla hiyo ambapo makampuni kadhaa ya Korea yalionesha ubunifu wa bidhaa zao.

Akipongeza Maadhimisho hayo  Mtafiti Mwandamizi Na Mshauri wa Masuala ya Siasa na Uchumi kutoka Ubalozi wa Korea hapa nchini, Hyunseok Jeon amesema maonesho hayo yamefanya kwa ushirikiano wa Watanzania kwa mara ya kwanza mwaka huu na kuweza kuonesha ubunifu wa bidhaa zao na hivyo kuweza kupanua wigo wao kiuchumi.


Miongoni mwa bidhaa zilizooneshwa kwenye maonesho hayo ni pamoja vipodozi, mitindo ya mavazi na utamaduni wao.












Sehemu ya watazamaji wakishuhudia ubunifu wa bidhaa ziulizokuwa zikioneshwa na Wakorea

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad