JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TADB YATOA TAARIFA YA MAENDELEO KATIKA UTENDAJI KAZI KWA ROBO YA PILI YA MWAKA

Share This

 

Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Frank Nyabundege akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Julai 29, 2024 wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya benki hiyo kwa robo ya pili ya mwaka.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo TADB Katika toleo la leo Julai 29, 2024 juu ya mahesabu ya benki hiyo imekuza mali (total assert) kutoka bilioni 612 mpaka shilingi bilioni 753 sawa na ukuwaji wa asilimia 23 katika robo ya pili mwaka iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Frank Nyabundege amesema kuwa TADB imetoa taarifa ya maendeleo ya Ukuaji wa Benki hiyo kwa miezi sita iliyopita au robo ya pili ya mwaka, kutokana na sheria ya Kibenki na Taasisi za fedha ya mwaka 2006 pamoja na kanuni zake za mwaka 2015 kwamba kila taasisi ya Kifedha nchini lazima itoe mahesabu yake na utendaji wake kazi kwa miezi sita iliyopita.

“Kwa kipindi kilichopita robo ya tulitangaza kuwa mali zilikuwa sh. Milioni 612 lakini kwa sasa zimekua hadi bilioni 753.” Amesema Nyabundege

Katika kuhakikisha watanzania wananufaika katika sekta ya Kilimo, Uvuvi na Sekta ya Ufugaji ambazo ni sekta zinazoajiri watu wengi zaidi Tanzania Nyabundege amesema TADB mikopo ya benki hiyo imekua kwa asilimia 38 kutoka sh. Bilioni 337 hadi sh. bilioni 466.7.

Kwa upande wa Faida Nyabundege amesema sehemu inayofanya taasisi iweze kujiendesha, ni faida ambapo kwa mwaka jana ilikuwa na faida ya shilingi. Bilioni 7.4 iliyoongezeka kwa asilimia 37 na kufikia shilingi bilioni 10. 2 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2024.

Amesema ukuaji huo wa faida ya TADB umetokana na utashi wa kisiasa ambao serikali ya awamu ya sita imekua nao juu ya watanzania walio katika sekta ya kilimo, Ufugaji na Uvuvi.

Amesema serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani ilijitanabaisha kwamba inataka kukuza Uchumi wake kupitia sekta ya kilimo.

Kwanza ilianza kukuza bajeti za kisekta ambazo ni sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi bila kuacha benki ya TADB.

“Selikali ilipoingia madarakani ilitoa mtaji kwa benki hiyo kwani ilikuwa na mtaji mdogo wa shilingi bilioni 60 tu. Na ilitoa mtaji wa sh. Bilioni 208 kwa mwaka 2021 na mwaka uliofuata wa 2022 210 kwa mwaka jana 2023 na kwa 2024 iliwaongezea mtaji wa sh. Bilioni 613.ambapo hizo ndio fedha serikali ilizoingiza katika benki hii.” Ameeleza

Nyabundege amesema kuwa malengo ya Rais Dkt. Samia ni kuwawezesha benki ya TABD ili iweze kutoa mikopo kwa watanzania wa Kima cha chini ambao ni wakulima, wafugaji pamoja na wavuvi.

“Serikali ya awamu ya sita inawajali watanzania na inataka kuhakikisha inatransform Maisha yao kutoka katika Maisha ya kima cha chini Kwenda kwenye Maisha mazuri.”

“Ukuaji wa TADB mpaka mpaka sasa unafikia sh. Bilioni 753. Hii inaifanya benki kuwa benki ya 15 kwa bora nchini kwani Tanzania inazaidi ya benki 45.

Kwa miaka 9 iliyopita benki imeweza kukua na kuzidi benki nyingi ambazo zimeazishwa miaka 25 na zaidi.

Pia Nyabundege amesema watahakikisha wanafika kwenye nafasi ya 10 bora za Mabenki nchini.

Katika Ukuaji huo TADB wameweza kukua na kufikia Nyanja za kimataifa na kuwa benki ya pili katika benki za maendeleo katika nchi zilizo mwanachama wa jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC). Kwasababu ya ukuaji, umuhimu wa kwa watanzania na ni watu wangapi wananufaika na mikopo na watu wangapi wanatoka katika dimbwi la Umasikini Kwenda kwenye Maisha bora.

Nyabundege amesema kuwa ukuaji huo wa TADB unatokana na kuwa na Rais anayewajali watanzania na anatumia taasisi zake kuhakikisha watanzania wananufaika kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wavuvi na wafugaji wadogo.

“Serikali ya awamu ya sita imeuongezea mtaji wa zaidi sh. Bilioni 54 ambapo mpaka sasa zimetolewa sh. Bilioni 37 kwahiyo jumla ya mtaji wa mfuko huo mpaka sasa ni bilioni 90. Licha ya kufikia bilioni 90 tayari mfuko huo umeshatoa mikopo kwa wanufaika ya sh. Bilioni 317 mpaka kufikia mwezi Juni 2024.

Mikopo hiyo imetolewa kwa kuashirikiana na taasisi za kifedha 19 za hapa nchini.”

Amesema huwa wanatoa dhamana na ukwasi ili kuimarisha benki za kibiashara kwani zimekuwa zikiona mikopo kwa wakulima, wavuvi na wafugaji wadogo ni hatarishi na wao wanawapunguzia hivyo viatarishi.

“Sasa mikopo imepungua kutoka asilimia 20- 36 ambazo zilikuwa zikichajiwa kwa miaka mitatu iliyopita. Mpaka sasa mikopo hiyo hutolewa kwa asilimia 9 hadi 14. Na hii pia kwa sababu tumekuwa na kiongozi anautashi wa kisiasa na kutambua kuwa wananchi wanaweza kunufaika kupitia taasisi za kifedha nchini.”

Amesema Mfuko huo umeweza kuwapatia mikopo wakulima, wavuvi na wafugaji wadogo 23659, lakini vyama vya ushirika 475 vyenye wanufaika 777,104 pamoja na wanaopata mtu mmoja mmoja tayari mfuko huo umewafikia wanufaika 765763. Kati ya hao wanawake ni asilimia 22.4 vijana ni asilimia 19.

“Kwahiyo TADB tumekuwa tukitenga fedha ili kuhakikisha wanawake na vijana wananufaika na mikopo hii ili wakulima, wavuvi na wafugaji wadogowadogo wanaweza kunufaika.”

Kwa kutenga mfuko huu umeweza kudhamini vijana na Wanawake nchini na umeweza kuwasaidia kujikwamua katika Uchumi wao.

Kwa sasa ukienda kwenye benki 19 ambazo wanashirikiana nazo wanatoa mikopo ya kilimo na dhamani inatoa TADB maana Rais Dkt. Samia amemwaga fedha kwaajili ya kusaidia wakulima wadogo, wavuvi na wafugaji.

MIKOPO KWA WAVUVI.
Nyabundege akizungumzia kuhusiana na Mikopo kwa Wavuvi amesema kuwa Rais Dkt. Samia alitoa fedha sh. bilioni 225 kwaajili ya Kwenda kusaidia vijana walio katika sekta ya uvuvi, kinamama na watu wote wanaofanya kazi ya Uvuvi katika Bahari na maziwa na mito, fedha hizo zitolewe bila riba yaani riba ni sifuri.

Amema fedha hizo zilitolewa kwaajili ya ununuzi wa boti za kisasa ambazo zinavifanya doria maalumu vinavyotafuta Samaki walipo badala ya kutumia boti za kawaida zisizo na vifaa maalumu ambavyo vitawasaidia kuvua Samaki kwa uharaka na urahisi.

Amesema mpaka sasa wameshatoa boti 156 za kisasa zambazo zina injini za kisasa pamoja na mafriza ambapo watakuwa wanaweka Samaki.

Boti hizo zimeshanufaisha watu 3213 kati ya hao 1099 ni wanawake ambapo kabla yah apo wanawake kumiliki bodi ilikuwa nikitu kigumu.

Mama Samia amesema wanawake wanastahili kumiliki Uchumi wa nchi hii ndio maana amewaletea fedha TADB ili wanawake wa nchi hii waweze kumiliki boti.

Pia ametoa wito kwa wanawake kutumia fursa hiyo kwani utawala wa awamu ya sita unajali wanawake, Vijana na wananchi wa kima cha chini kwani anawapa kipaumbele.

VIZIMBA
Nyabundege akizungumzia kuhusiana na Vizimba amesema kuwa bado wanaendelea katika utekelezaji wa vizimba lakini tayari vizimba 117 vimeshatolewa kwa wanufaika 674 kati ya hao 161 ni wanawake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad