JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Shule Daarul- Arqam yajengea maadili vijana---Meneja Bakari Yahya anena

Share This


-Asema sera mpya ya elimu kuwatoa vijana vijiweni

-Aahidi Shule yake kuendelea kuwa bora hapa Jijini na Nchini

Mwandishi Wetu

Shule ya Msingi Daarul- Arqam iliyopo Kigamboni Kitongoji cha Cheka imekusudia kujenga taifa lenye maadili mema miongoni mwa vijana wa Kitanzania Meneja wa Shule hiyo Bakari Yahya anasema kuwa shule yake inafundisha wanafunzi wake juu ya maadili na hofu kwa Mungu katika kuandaa kizazi bora kichajo.

Yahya anasema "Tunaandaa vijana au viongozi wa baadaye wenye hofu ya Mungu ambao itakuwa vigumu kufanya ubadhirifu wa rasilimali za nchi na ambao wataliongoza taifa hili kwa uadilifu "

 Anasema shule yake inafundisha masomo kwa kufuata Mtaala wa serikali , lugha ya Kiarabu na kuhifadhi Quraan Tukufu miongoni mwa wanafunzi wake, Shule hiyo inaanzia Elimu ya Awali, Shule ya Msingi na Sekondari na ina mazingira mazuri ya watoto kujifunzia ikiwa na madarasa ya kutosha ndani ya eneo kubwa sanjari na mabweni ya kutosha.

Anasema shule yake imekuwa ikifanya vizuri katika hatua mbalimbali za mitihani na kwamba anatoa wito kwa Watanzania kupeleka wanafunzi shuleni hapo kwa uhakika wa elimu bora, maadili mema na uvumbuzi wa vipaji ukiambatana na masomo ya michezo, kwani anasema michezo ni afya, michezo ni kichocheo cha kijana kufanya vizuri masomoni.

Anasemaje kuhusu sera mpya ya elimu? Yeye anaipongeza hiyo inayotilia mkazo elimu kwa vitendo kwani itasaidia kujenga uwezo kwa vijana kujiajiri na pia kajiriwa.

"Naipongeza serikali kwa sera ya elimu ambayo inatilia mkazo mafunzo kwa njia ya vitendo zaidi na kwamba itawapa vijana uwezo wa kijiajiri pindi wamalizapo elimu ya sekondari au zaidi,"  

"Kwa shule ya msingi tumeshaanza kutekeleza sera hiyo na tunaendelea kujiandaa kwa upande wa sekondari na kwamba baada ya muda mfupi tutaanza utekelezaji," anasema.

Anaongeza kuwa sera hiyo itawaondoa vijana vijiweni kwani baada ya kuhitimu masomo yao kwa hatua mbalimbali sasa wataweza kujiajiri.

Kwa Mawasiliano zaidi na Shule 0718999777.

Meneja wa Shule hiyo Bakari Yahya
 Mandhari  mwanana ya Shule hiyo
Baadhi ya wanafunzi wa Shule hiyo



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad