JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Serikali Yatangazia Kiama kwa Wadanganyifu Vyuo vikuu

Share This

 


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda kulia akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 12,2024 jijini Dar es Salaam juu ya tuhuma za udanganyifu kwenye mitihani  ya vyuo vikuu nchini.  Kushoto ni Katibu Mkuu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu  (TCU) Profesa Charles Kihampa

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv.
SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuwabana wanafunzi watakaofanya mitihani kwa njia ya udanganyifu na kuwachukulia hatua kali ili kudhibiti na kulinda mfumo wa elimu.

Hayo yamesemwa leo Julai 12, 2024 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda , alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari juu ya tuhuma za udanganyifu kwenye mitihani.

“Hivi karibuni kulikuwa na tuhuma zinarushwa na vyombo vya habari kwamba kuna udanganyifu kwa baadhi ya vyuo vikuu hasa kwenye mitihani, tuhuma hizi zinavyosemwa zinaweza kusababisha watu kudhani hali ya vyuo vyetu vikuu ni mbaya hivyo napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa vyuo vyetu vikuu vinazingatia maadili na uweledi hasa katika mitihani kuhakikisha kwamba tunatoa shahada kwa mujibu wa taratibu zinazokubalika katika taaluma zetu” amesema Profesa Mkenda.

Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa dalili za udanganyifu elimu ya juu nchini bado ina ubora wa hali ya juu “suala la udanganyifu na majaribu ya udanganyifu yapo dunia nzima kwa nchi zote suala kubwa ni mbinu zinazotumika kuzuia udanganyifu pamoja kuwa tunaendelea vizuri lakini upo usemi kila tunaposikia tuhuma kwa kweli sisi tunachukulia ni jambo kubwa na zito”.

“Niwakumbushe kulikuwa na dalili kama hizo katika mitihani ya darasa la saba , kidato cha nne na kidato cha sita tulichukua hatua kali kwa bahati mbaya ziliumiza maslahi ya baadhi ya wawekezaji kwenye sekta ya elimu lakini pamoja na mashinikizo na lawama tulichukua hatua kwa sababu udanganyifu una madhara makubwa na kunaondoa usawa pia kunadhoofisha elimu.

Profesa Mkenda amesema kuwa Serikali haitaingilia mamlaka ya vyuo vikuu “Juzi wamehukumiwa baadhi ya watuhumiwa wa udanganyifu wa mitihani kuhusu vyuo vikuu kuna utaratibu wake wa kusimamia mitihani , chuo kikuu mtu akidanganya kwenye mitihani ni kufukuzwa vyuo mimi pale ofisini kwangu kuna malalamiko ya wazazi ambao watoto wao walifukuzwa chuo nikifuatili naona taratibu zimefanyika nami kama Waziri nimekataa kuingilia mamlaka ya vyuo vikuu wanapochukua hatua kama hizo kwa sababu tunalinda masuala ya mitihani’’

Akizungumzia suala la wanafunzi wa Chuo Kikuu huria lililosambaa hivi karibuni la kuonekana kuwa wanafunzi wanafanyiwa mitihani “juzi hapo Open University kugundua watu waliokuwa wanataka kufanyiwa mitihani ni jitihada zinazoendelea vyuo vyote

Amesema kwa mfano vyuo mtu akienda kufanya mtihani lazima aende na kitambulisho chake chenye picha ni marufuku kuingia na simu ukikutwa unafukuzwa chuo watu wanalalamika tumekuwa wakali kwa hiyo litaendelea na majaribio ya udanganyifu duniani yataendelea na sisi tutaendelea kuwabana”

Waziri Mkenda ameendelea kusema kuwa, serikali imefanya uchunguzi juu tuhuma zilizoanikwa na moja ya chombo cha habari nchini kwamba kuna mwanafunzi alihonga ili abadilishiwe matokeo kwenye mfumo wa tehema.
“Nilimemwambia Katibu Mkuu aunde tume huru kwenda kuchunguza ikiwa pamoja na idara ya usalama wa Taifa walioambatana na wataalamu wa tehema walifanya uchunguzi kwenye mifumo ya tehema waliingia wakaangalia mfumo wote na uzuri kwenye mfumo ni rahisi kuona mtu aliyengia na kufanya mabadiliko ameingia saa ngapi tuligundua kuwa zile tuhuma ni za uongo na yule aliyetuhuma hizo hajajitokeza inaonekana watu wanataka nafasi ya Kaimu Mkuu wa Chuo ambaye anakaribia kustaafu“.

Profesa Mkenda amesema kuwa serikali itaendelea kudhibiti njia zote za udanganyifu bila kuingilia mamlaka ya vyuo pale wanapochukua hatua kwa wadanganyifu.

Amesema kuwa utetezi wa wanafunzi wanaohitimu PHD na Masters lazima wateteePHD zao hadharani itatangazwa siku ya mtu huyo anayokwenda kutetea taaluma yake hadhari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad