JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ONGEZEKO LA VIWANDA MKOANI PWANI LITAPUNGUZA UAGIZAJI WA BIDHAA NA MALIGHAFI NJE YA NCHI-RC KUNENGE

Share This

 






Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
MKUU wa mkoani Pwani, alhaj Abubakar Kunenge amejinasibu kuwa ongezeko la viwanda mkoani humo litaongeza uzalishaji wa bidhaa na malighafi hali itakayosaidia kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo nje ya nchi.


Kutokana na mafanikio hayo, azielekeza Taasisi wezeshi kuondoa ukiritimba kwa wawekezaji badala yake watumie nafasi zao kuwaelekeza taratibu zinazotakiwa ili kufikia malengo waliyowekwa.


Kunenge alieleza hayo wakati alipotembelea kiwanda cha Vioo KEDA Tanzania ,kata ya Mbezi, Mkuranga mkoani Pwani, ambacho hadi kukamilika kitagharimu fedha ya kimarekani 309,000,000usd ikiwa ni sawa na fedha ya kitanzania sh.bilioni 803.4.


Mkuu huyo wa mkoa, alieleza , mkoa huo hadi sasa una viwanda 1,535 kati ya hivyo vikubwa ni viwanda 124.


Kunenge alisema, Serikali inaendelea kushirikiana na wawekezaji ili kuinua uchumi wa mkoa na Taifa kijumla.



Alifafanua, uwepo wa viwanda utasaidia ongezeko la ajira, kuongeza pato la Taifa sanjali na kukuza sekta ya viwanda nchini.


Vilevile alizisisitiza, wilaya kusimamia mipango mji kwa kutenga maeneo ya viwanda hatua itakayosaidia kuondoa migogoro ya ardhi kati ya wananchi na wawekezaji wa viwanda.


Awali akitoa taarifa ya mradi, Ofisa biashara Ruby Zhu alisema, ujenzi wa mradi ulianza march 2023, mradi upo awamu kwanza ambapo utakamilika baada ya miezi 18 na awamu ya pili itaanza mwaka 2027.


"Wiki mbili ijayo tutafanya majaribio ya mashine na kupata gesi, na mwezi wa tisa wataanza uzalishaji ambapo kila siku watazalisha tani 600 na kwa mwaka watakuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni 219." alisema Ruby.


Ruby alieleza, wanatarajia kuwa na ajira zaidi 1,600, walianza uwekezaji mkoani Pwani kwa kuwekeza kiwanda cha marumaru Chalinze, Kiwanda cha taulo za watoto,sabuni KEDS Kibaha Mjini na Kiwanda cha Vioo Mkuranga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad