JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


NIC yaweka mikakati ya kulinda Uwekezaji nchini

Share This

 





Mkurugenzi Mtendaji  wa NIC Insurance  Kaimu  Mkeyenge akiwa katika Maonesho ya Sabasaba katika Ofisi ya NIC Insurance na baadhi ya Wadau kwa moja kwa moja na NIC.

*Kutokana na Bima zao kwa kulipa fidia ya majanga kwa wakati.

Na Chalila Kibuda
Mkurugenzi mtendaji wa NIC Insurance NIC Kaimu Abdi Mkeyenge amesema kufuatia uwekezaji unaondelea nchini wawekezaji wanapaswa kukata bima za biashara zao ili pindi majanga yanapojitokeza waweze kufidiwa kwa wakati na kuendelea kuzalisleo

NIC ipo kwa ajili ya Biashara hivyo baada ya uzalishaji wote tunatoa gawio ili Serikali iendelelee kutekeleza miradi yake kwa wananchi.

Akizungumza leo Dar es salaam mara baada ya kutembelea kwenye banda la NIC lilipo kwenye maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa amesema shirika limekuwa likitoa bima mbili muhimu kwa ustawi wa nchi.

Akizitaja Bima hizo amesema ni Bima za Maisha na Bima sizizo za maisha ambapo bima zisizo za maisha zinaenda moja kwa moja na kauli mbiu ya maonesho hayo isemayo Tanzania mahali salama pa biashara na uwekezaji'

"NIC hili ni shirika la umma hivyo tunatoa bima aina mbili za maisha na zisizo za maisha ambazo hizi zinawagusa moja kwa moja wawekezaji kwani mwekezaji akipata majanga tunaweza kuwafidia na wakaendelea na uwekezaji wake kama kawaida na kufanya nchi iweze kuendelea kwa uchumi ",Amesema.

Amesema pamoja na kuwa ni Taasisi ya serikali lakini pia wanafanyabishara kwani wanajukumu la kulipa kodi lakini wanajukumu kubwa la kuwahudumia Watanzania.

Akizungumzia mikakati waliojiwekea katika mwaka huu wa fedha kuhusu kutoa uelewa kwa wananchi amesema wamejipanga kuwafuata wananchi walipo na kuwapa elimu ya Bima ili kufikia kiwango kikubwa cha watumiaji wa Bima nchini.

Tulichogundua wananchi wengi hawana elimu ya bima sasa tumejipanga kuhakikisha tunawafuata huko huko walipo na kuwapa elimu hii maana bima ni muhimu na uwezi kuona umuhimu wake kama hayajakukuta sasa hatusubiri yakukute tutahikikisha elimu inamfikia kila mmoja ili waweze kujiunga na Bima",Ame

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad