JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Naibu Spika Zungu Mgeni Rasmi Mahafali ya Chuo cha Furahika

Share This




Ni Jitihada ya Rais Dkt.Samia Suluhu ya mpango wa Elimu Bure

NA MWANDISHI WETU

Mahafali ya 19 ya Chuo Cha Ufundi Stadi cha Furahika ambacho kipo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam yanatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi Naibu Spika Mussa Azzan Zungu

Mahafali hayo yanatarajiwa kufanyika Agasti 3 mwaka huu katika Viwanja vya St.John Buguruni Malapa Jijini Dar es Salaam yakiwa yakiwa na Wahitimu 120 wa kozi mbalimbali ikiwemo Ualimu, Sekretari, Hoteli na nyinginezo ambazo zipo chini ya VETA na mhitimu ambaye amefanya vizuri kwa kila kozi atapewa zawadi kama ilivyo kawaida.

Mahafali hayo kuwa na Mgeni Rasmi Naibu Spika kuonyesha jitihada za Chuo hicho ili kuweza kujionea mafanikio ya vijana katika kupata elimu bure ikiwa ni kuunga jitihada za Serikali ya awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan

Hayo ameyasema Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya jijini Dar es Salaam huku akiwaomba wazazi na walezi wa vijana hao wanahitimu na wengineo kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo muhimu katika maisha ya watoto wao.

“Furaha kubwa kwenda kusheherekea Mahafali ya 19 tangu chuo hiki kianzishwe na mgeni wetu ataakuwa Mbunge wa Ilala, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu, hivyo tunawaomba wazazi ama walezi wa vijana ambao wanahitimu mafunzo haya waje kwa wingi kufurahia kwa pamoja na watoto kwa siku hii muhimu kwa maisha yao.

“Pia mahafali haya yanafungua milango kwa kundi lingine kujiunga na muhula mpya wa masomo kwa miezi sita na mwaka mmoja kwa kozi ya hoteli, Bandari na nyinginezo na tunawaomba vijana ambao wameishia darasa la saba, kidato cha pili ama kidato cha nne na wakashindwa kupata alama nzuri za kuendelea na masomo waje hapa kutimiza ndoto zao katika elimu,” amesema

Ameongeza kuwa muhula mpya utaanza Septemba 10 mwaka huu pamoja na kozi mpya ya Uhariri na upigaji picha za video (Video Production) itaanza kufundishwa chuoni hapo jambo linalotanua wigo wa vijana wengi kutimiza ndoto zao kwa kupata ujuzi wa kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Amesisitiza kuwa yote yanafanyika kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufungua milango ya uwekezaji na kusababisha mashirika mengi kuja kusaidia vijana na wao kutoa elimu bure na jambo linalitakiwa sasa ni vijana kutumia fursa hiyo vizuri ili kujikomboa katika dimbwi la umasikini.

Dkt Msuya ameongeza kuwa wanafunzi ambao wanajiunga na chuo hicho wanapata fursa ya kutafutiwa sehemu ya mafunzo kwa vitendo na wale wanaofanya vizuri wanajiweka katika mazingira mazuri ya kupata ajira baada ya kumalizi masomo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad