JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MTANDA AZINDUA TIKETI ZA PAMBA DAY AKIUZA TIKETI ZAIDI YA 5,000

Share This

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Said Mtanda, akizungumza na waandishi wa habari wakiwemo wadau,viongozi wa soka na mashabiki wa Pamba Jiji,leo akizindua uuzwaji wa tiketi za Pamba Day. 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Said Mtanda (mwenye miwani kulia),akizindua uuzwaji wa tiketi za viingilio vya Tamasha la Pamba (Pamba Day) leo kwa kukata utepe.

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
MKUU wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda,leo amezindua uuzwaji wa tiketi za kuingilia katika Tamasha la Pamba Day na kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu ya Pamba Jiji kuwahi mapema kununua tiketi zao ili kuwahi nafasi.


Akizindua uuzwaji wa tiketi hizo katika Uwanja wa Nyamagana,uliofanyika sambamba na mkutano wa wadau kutoa maoni kuhusu Pamba Jiji,amesema zitatumika kuingilia uwanjani kushuhudia tamasha hilo la aina yake kuwahi kufanyika mkoani humu.


Mtanda amesema tamasha la Pamba Day linatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, Agosti 10 mwaka huu,zimetengenezwa tiketi 25,000 na kuwataka washabiki na wananchi kuwahi kununua tiketi kabla nafasi hazijaisha.


Amesema serikali ikishirikiana na uongozi wa Pamba Jiji imedhamiria kurejesha heshima ya Mwanza katika soka na furaha ya mashabiki wa timu hiyo almaarufu Tour Poissant Lindanda wa ndani na nje ya nchi waliyoikosa kwa zaidi ya miaka 23.


Mtanda amewashukuru wachezaji wa zamani waliopo na waliotangulia mbele za haki,bodi kwa usimamizi ulioiwezesha timu kuingia kambini kujiandaa kwa msimu na sasa ni wakati wa watu wenye maoni ya kuboresha timu wauone uongozi ili watoe maoni hayo.


Mkuu huyo wa mkoa pia amemshukuru Mwenyekiti wa timu hiyo, Bhiku Kotecha,Menejimenti ya Jiji,mashabiki, wapenzi na wananchi wa Mwanza kwa ufanikisha Pamba Jiji kucheza ligi kuu msimu wa mwaka huu.


“Kazi iliyobaki ni kumlea mtoto Pamba Jiji,wenye kuisadia na kushusha ni wana Mwanza wenyewe,wapo watakaozipokea timu pinzani na kufichua siri ya kambi ya timu,wanatamani kuona migororo wajinufaishe, siku za mechi kwenye msimu ujao wakajitokeza watu kuwapokea wageni” amesema na kuongeza;


“Tusiwe wa kwanza kushusha timu yaliyo matamanio ya walio wengi na siyo matamanio ya wachache wanazipokea timu pinzani za nje ya mkoa, hatutakubali mtu wa kuvuruga na hatutaoneana haya,kama noma na iwe noma,tuendelee kuiunga mkono Pamba Jiji.”


Mtanda amesema Pamba Jiji ni mali ya wadau kila mmoja ana haki ya kuipgania hata kwa matambiko na maombi ili timu ifanye vizuri, hivyo waipe ushirikiano wa kutosha.


Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa timu hiyo imekamilika sababu usajili uliofanywa ni mzuri kutokana na mchujo wa wachezaji zaidi ya 900, pamoja na usajili wa wachezaji kutoka nje wapo wazawa katika kikosi hicho maarufu kama Wana Kawekamo.


Tamasha la siku ya Pamba (Pamba Day) litatumbuizwa na wasanii mbalimbali wanaotokana na Mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Fid Q au Farid Kubanda, Harmonize na wengine wengi.


Aidha kutakuwa na tiketi za sh.100,000 kwa jukwaa la V-VIP, Sh.50,000 kwa VIP,sh.10,000 na sh. 3000 mzunguko ambapo tayari zaidi ya tiketi 5,300 zimeshauzwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Said Mtanda (mwenye miwani kulia),akizindua uuzwaji wa tiketi za viingilio vya Tamasha la Pamba (Pamba Day) leo kwa kukata utepe.
Wadau na wananchi wakifuatilia uzinduzi wa tiketi za Pamba Day, leo katika Uwanja wa Nyamagana.
Mashabiki wa soka wakiwemo wa Pamba Jiji wakifuatilia tukio la uzinduzi wa tiketi za Pamba Day leo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pamba (Pamba Day),Amina Makilagi,akizungumza leo katika Uwanja wa Nyamagana.
Meya wa Jiji la Mwanza na Mwenyekiti wa Bodi ya timu hiyo,Costantine Sima akizungumza,leo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda (kulia),kuzindua uuzwaji wa tiketi za Pamba Day.
Picha zote na Baltazar Mashaka

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad