JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Mkeyenge:Tumejipanga kuwahudumia Wawekezaji nchini

Share This
Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi akimkabidhi tuzo ya mshindi wa Kwanza katika katika kundi la watoa Bima nchini Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge  wakati wa Kilele cha Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa (DITF) yaliyofungwa na Rais Dkt.Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC insurance Kaimu Mkeyenge akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuibuka na ushindi wa kwanza katika kundi la Kampuni za Bima katika Kilele cha Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa (DITF) yaliyofungwa na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Kaimu Mkeyenge akizungumza na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Karim Meshack katika Banda la NIC alipotembelea baada ya kufungwa Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa (DITF)

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa NIC insurance  Karim Meshack akiwa katika picha pamoja na timu ya NIC Insurance iliyokuwa ikihudumia wananchi katika Maonesho ya 48 Biashara Kimataifa  yaliyofungwa  na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi.


*Wawekezaji hao ni matokeo ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuitangaza nchi katika Mataifa mbalimbali

Na Chalila Kibuda ,Michuzi Tv
MKURUGENZI Mtendaji wa NIC insurance Kaimu Mkeyenge amesema NIC imejipanga katika kuhudumia wawekezaji nchini.

Wawekezaji hao ni juhudi zilizofanywa na Rais Dkt . Samia Suluhu Hassan ya kuitangaza Tanzania ambapo wawekezaji waliofika na wanaondelea NIC itaendelea kuwahudumia

Mkeyenge ameyasema wakati akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ngao ya ushindi wa kwanza wa utoaji wa bima kwenye Kilele cha Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa (DITF) yaliyofungwa na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi.

Mkeyenge amesema kuwa kauli mbiu ya Maonesho Tanzania ni Mahali Sahihi ambapo NIC ni kwenda kuhakikisha Uwekezaji huo Bima inakwenda kutoa kufikiria majanga watayokutana mara baada ya Uwekezaji.

Aidha amesema kuwa katika mikakati yake yao ni kwenda kukatana na wadau wa Uwekezaji kuwapa elimu juu ya Bima na faida zake.

Mkeyenge amesema kuwa wana bidhaa nyingi za Bima ambazo zinatakiwa zikatwe kwa wananchi na wawekezaji.

Hata hivyo amesema NIC ni Taasisi ya Serikali katika kufanya kazi inatoa gawio linalokwenda kuhudumia wananchi kwenye miradi mbalimbali inayotekelezwa.

Amesema katika kipindi cha sasa Bima zina umuhimu kwani majanga yakitokea kimbilio ni Bima kwa ajili ya kufidiwa kwa muda mwafaka.

Mkeyenge ameyasema kuwa wana mifumo ya Tehama imara ambapo wateja wanapata huduma moja kwa moja walipo pamoja na madai ni ndani ya mfumo wa Tehama.

Amesema katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Dkt.Samia Suluhu Hassan wamekuwa na mafanikio katika utendaji wa kuhudumia wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad