JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Minja kukata rufaa kupinga kuachiwa kwa mfanyakazi wa benki

Share This

 


Na Mwandishi Wetu
MFANYABIASHARA Deogratus Minja amewasilisha kusudio la kukata rufaa dhidi ya mfanyakazi wa benki, Ibrahim Masahi (40) katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam kupinga hukumu iliyotolewa ya kumuachia huru mfanyakazi huyo kwenye kesi ya kujeruhi.


asahi ambae ni jirani yake Minja anatuhumiwa kumpiga kwa kutumia nyundo jirani huyo na kumsababishia kupata madhara makubwa ya mwili mwake kwa madai kuwa kwanini alikwenda kumshtaki serikali za mtaa kwamba anatililisha maji machafu.

Minja amefikia hatua hiyo, kwa kile alichodai kuwa ushahidi aliyoutoa mahakamani kwenye kesi namba 100 ya mwaka 2023 haukusomwa kwenye hukumu ambayo ilimuachia mshtakiwa huyo.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi, Amos Rweikiza amesema kuwa ushahidi uliyotolewa na mashahidi wanne wa upande wa mashtaka haukuweza kuthibitisha kesi bila kuacha shaka lolote.

Amesema kutokana na ushahidi uliyotolewa na Minja ni kweli alijeruhiwa na aliweza kuonesha majeraha mbele ya Mahakama na pia hata daktari aliyemchunguza alieleza jinsi mlalamikaji alivyokuwa amejeruhiwa.

Hakimu Rweikiza amesema katika kiini kama mlalamikaji aliweza kumtambua mshtakiwa?, kwa sababu ushahidi unaonesha tukio hilo lilitokea nyakati za usiku na mlalamikaji alidai alipigwa akadondoka chini ndipo akamgeukia akamtambua mlalamikiwa.

"Kuna haja kutengeneza utambuzi kama alimtambua kwa ufasaha, kwenye ushahidi wa Minja alisema mshambuliaji alisimama

nyuma yake akampiga na tukio lilitokea usiku, kisheria lazima aseme kulikuwa na mwanga kiasi gani ambao ulimsaidia kumtambua,"

"Kwenye kutambua mtu aliyeshambuliwa ili aweze kumtambua mtu sawa, lazima aseme ukubwa wa mwanga, kwenye ushahidi wake Minja hakutaja kabisa chanzo cha mwanga ambao alikitumia kumtambua mtuhumiwa,"amesema Hakimu Rweikiza

Pia, Hakimu Rweikiza amesema wakati mlalamikaji anaulizwa maswali ya dodoso na Wakili wa Utetezi Nestory Wandiba, alidai kuwa ni tukio hilo lilitokea muda mfupi sana, kwa hiyo suala la utambuzi lazima lielezewe kwa ufasaha.

"Katika ushahidi haikuwekwa wazi kama ni nani alimsaidia mtendewa baada ta tukio kutokea kama ni mama Emma au Fadhili.

Utambuzi uliyofanywa na mtendewa haujakidhi vigezo vya kisheria na umeacha mashaka,"

"Kesi haikuthibitishwa kwa viwango vinavyotakiwa katika ushahidi, utambuzi wa mtendewa hakuwa sawasawa kulitakiwa kuwepo na shahidi mwingine ambae angelionesha hilo,"amesema

Wakati akijitetea, Masahi amedai kuwa hana mahusiano mazuri na jirani yake Minja takribani miaka nane ndiyo maana amembambikia kesi ya kumjeruhi mwili wake na pia ni kweli alimkuta mlalamikaji akiwa amesimama na shemeji yake nje ya geti la nyumbani yake siku ya tukio.

Masahi alikuwa akituhumiwa kwamba Januari 11, 2023 akiwa eneo la Mbezi Msakuzi ndani ya Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam alimshambulia na kumjeruhi Deogratus Minja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad