JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Kesi Ya Wanandoa ,Wakili Aomba kumuhoji tena Daktari

Share This

 

Na Mwandishi Wetu
UPANDE wa utetezi katika kesi ya kujeruhi na kutoa lugha chafu ya matusi inayowakabili wanandoa Bharat Nathwan na Sangita Bharat umeiomba Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu iwaruhusu kumuita tena shahidi namba moja katika kesi hiyo Dkt. Lucia Rumoyi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja ili ahojiwe kwa nini aliandika ripoti ya wagonjwa wakati akijua hajasajiliwa na baraza la madaktari nchini.

Wakili Edward Chuwa anayewatetea watuhumiwa hao, aliwasilisha maombi hayo hivi karibuni mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiendelea kwa hatua ya ushahidi.

Hatua ya Wakili wa Utetezi, Chuwa kuomba kumuhoji shahidi huyo ni kutokana na wasiwasi wao ya kwamba Lucia Rumoyi sio daktari kutokana na kutosajiliwa na baraza la madaktari.

Alidai licha ya shahidi huyo kujitambulisha kuwa yeye ni Daktari lakini walipofiatilia walikuta hajasajiliwa kwenye baraza la madaktari.

Hata hivyo uamuzi wa kama shahidi huyo ataitwa tena au la bado haujatolewa kufuatiwa wakili Chuwa kuwa na majukumu mengine na hivyo kuomba kesi hiyo iahirishwe hadi Agosti 6, 2024 kesi hiyo itakapokuja kwa ajali ya shahidi Kiran Larit kuhojiwa na upande wa utetezi.

Awali katika ushahidi wake Dkt. Lucia (52)akiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi Grace Mwanga alijitambulisha mahakamani hapo kuwa yeye ni daktari wa Hospitali ya Mnanzi Mmoja.

Alidai kuwa Julai 21,2023 alikuwa Idara ya Dharula chumba namba 20 muda wa mchana alipokea wateja wawili wenye asili ya kiashia ambao walikuwa wamechafuka kuanzia kichwani hadi miguuni , mama alichafuka sana kuliko baba

Alidai kuwa alianza kumuhudumia mama (Karan) kwa kumnawisha na maji ya dripu kwa sababu macho yake yalikuwa yanatoa machozi na pia alikuwa akilalamika kwamba ana maumivu makali na kichwa,.alikuwa akilalamika kuhusina na kichwa alimuuita daktari wa macho ili aweze kumuangalia.

"Daktari alibaini kwamba jicho la upande wake wa kushoto limepata madhara sana ,mgonjwa akaomba aandikiwe rufaa ya kwenda hospitali ya Regency ili aweze kupata matibabu kutokana na kwamba hapo hakuna vifaa vyakufanya uchunguzi, baada ya hapo tulimrudisha chumba namba 20, akachomwa sindano ya maumivu,"alidai Dkt. Augustino

Dkt. Augustino alidai kuwa alimuangalia mwili mzima, alikuwa ana mamumivu kwenye masikio, macho na kichwa ndipo akamuandikia rufaa, akaondoka nikaanza kumuhudumia baba (Kiram) ambapo alikuwa akilalamika kuwa anaumwa sana kichwa, kizunguzungu na anaona maluwe luwe baada ya kushambuliwa .

Alidai kuwa alimchunguza hadi kwenye miguu, alibaini kwamba alikuwa amevimba kichwani upande wa kulia, kifuani na pia magoti yake yalikuwa yamechubuka, nilimuandikia sindano za kupunguza maumivu na pia nilimuandikia akafanye vipimo vya CT Scan.

"Licha ya kumchoma sindano ya maumivu bado alikuwa anajisikia muamivu makali, ndiyo akaomba aandikiwe rufaa ya kwenda Regency kwa ajili ya uchunguzi zaidi,"alidai

Baada ya kumaliza kuwapa huduma zote,walienda kufanya vipimo wakamletea ripoti mbili. Kiran alirudisha ripoti ya CT Scan kutoka kitengo cha koo, masikio na macho.

Dkt Lucia alidai kuwa ripoti ilionesha kuwa kutokana na kemikali aliyopata katika macho alipata ugonjwa wa jicho na ubongo wake umepata mtikisiko, baada ya hapo alijaza fomu ya polisi Pf3.

Alidai kuwa madhara ambayo anaweza kuyapata ni kupata upofu na pia kidonda chake kinachukua muda mefu kupona sio wiki wala mwezi kwa sababu kina pona taratibu.

Pia, wagonjwa hao walipata maumivu ya nyama laini, tatizo hilo walitibiwa Mnanzi Mmoja, baada ya hapo alijaza Julai 21,2023.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, washitakiwa hao ambao ni raia wa India wanaoishi Mrina - Kisutu, Dar es Salaam wanaotuhumiwa kwa mashitaka manne waliyoyatenda Julai 21,2023.

Katika shitaka la kwanza la kujeruhi linalomkabili Nathwan peke yake, ambapo anatuhumiwa Julai 21,2023 akiwa eneo la Mrina-Kisutu ndani ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kinyume cha sheria alimsababishia madhara makubwa Kiram Abdallah kwa kuzamisha kichwa chake kwenye chokaa.

Pia, katika shitaka la pili la shambulio la mwili linalomkabili Nathwan peke yake, ambapo tarehe hiyo na eneo hilo alimsababishia madhara Lalit Kanabar katika mwili wake kwa kumpiga ngumi na mateke kichwani.

Ilidaiwa kuwa katika shitaka la tatu na la nne linalomkabili Sangita peke yake, ambapo anatuhumiwa kutoa matusi makubwa dhidi ya Abdallah na Kanabar kitendo ambacho kilileta fujo kwa namna ambayo inaweza kuleta uvunjifu wa amani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad