JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KAMPUNI 100 KUTOKA CHINA ZAJA NCHINI KUTAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI

Share This



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo  akizungumza wakati wa Kongamano la Wawekezaji na Wafanyabiashara lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na ubalozi wa Tanzania nchini China lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2024.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri akizungumza wakati wa Kongamano la Wawekezaji na Wafanyabiashara lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na ubalozi wa Tanzania nchini China lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kongamano la Wawekezaji na Wafanyabiashara lililofanyika jijjini Dar es Salaam leo Julai 30, 2024.
Balozi wa Tanzania nchini China, Khamis Mussa Omar akizungumza wakati wa Kongamano la Wawekezaji na Wafanyabiashara lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na ubalozi wa Tanzania nchini China lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri akizungumza wakati wa Kongamano la Wawekezaji na Wafanyabiashara lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na ubalozi wa Tanzania nchini China lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2024.


Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
MKAPUNI 100 za Nchini china zaja nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika sekta za viwanda, kilimo, utalii, madini na misitu.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2024 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema ujio wa wawekezaji kutoka china ni fursa kwa uchumi wa Tanzania.

“Nimeshazungumza na wawekezaji 100 waliotua nchini wakitokea China kuhusu fursa zilizopo ikiwemo kwenye viwanda, kilimo, utalii, madini na misitu ili wawekeze.”

Akizungumza wakati wa Kongamano la Wawekezaji na Wafanyabiashara lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na ubalozi wa Tanzania nchini China Prof. Kitila amesema kuwa kongamano hilo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China. 

Akizungumzia kuhusiana na Mawazo yasiyofaa kuhusu bidhaa za China amesema kuwa "Bidhaa nyingi zinatoka China na sisi kama nchi tunaviwango vyetu vya bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa na kampuni za kichina tunahakikisha kuwa zinakuwa na ubora".

Aidha amewataka Watanzania kushirikiana na wawekezaji hao wa kigeni ili wapate mitaji pamoja na teknolojia:"Tumeweka utaratibu mzuri kama Mtanzania unayo ardhi basi utashirikiana na mgeni ambaye anamtaji".Ameeleza Prof. Kitila

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri amesema ujio wa kampuni hizo za uwekezaji ni fursa kwetu kama nchi.

"Wakishirikiana na Watanzania watazalisha bidhaa zinazohitajika ndani ya nchi ikiwemo za usindikaji wa mazao ya kilimo, na bidhaa za ujenzi," amesema.

Amesema Watanzania wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo kwa kushirikiana na wawekezaji hao ambapo zitapatikana bidhaa za kuuza nje, kuanzisha kampuni, kodi zitalupwa na ajira zitapatikana.

“TIC tumeshirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na Ubalozi wa Tanzania nchini China kuwaalika Wafanyabiashara wengine 100 wa hapa nchini kwaajili ya kushirikiana na Wafanyabiashara wa Nchini China kufanyabiashara za mashirikiano.”

“Wawekezaji hawa wamekuja katika sekta tofauti tofauti ambazo ni Nishati, amabapo wanaaangalia uzalishaji wa vifaa na bidhaa zinazo zinazofanikisha umeme wa jua, sekta ya Viwanda ambapo wanajikita katika viwanda vya ujenzi, Viwanda vya usindikaji vyakula mfano Viwanda vya usindikaji wa Kahawa Pamoja na Katani, pia wamekuja wawekezaji wa Ujenzi pamoja na sekta ya Madini.” Amesema Teri

Pia amewaalika watanzania kushirikiana na kuanzisha kampuni, kuwekeza na kushirikiana pamoja kwajili ya manufaa ya watanzania kwa Ujumla.

Amesema TIC inatambua mchango wa China kwa kuwa wanamitaji mikubwa kwaajili ya uwekezaji wao hapa nchini ambapo wakishirikiana na watanzania wataleta matokeo Chanya kwenye uchumi wa nchi.

Teri akizungumza kuhusiana na ongezeko la Wawekezajia katika Serikali ya Awamu ya sita amesema ushiriki wa Watanzania wamekuwa wakiongezaka katika miradi ya maendeleo nchini.

“Katika mwaka uliopita TIC imesajili miradi 707 ambayo ni  ongezeko la asilimia 91 kutoka miradi 362 ambayo tulisajiri katika mwaka wa fedha 2022/2023 na katika miradi hii takribani asilimia 38 ni ya Watanzania, asilimia 20 ni miradi ya ushirikiano kati ya Watanzania na wageni. Miradi hiyo yote inamkono wa watanzania, ndio lengo la Rais Dkt. Samia alilokuwanalo alipoweka sheria ya uwekezaji yam waka 2022 kwamba ongezeko la watanzania wanaomiliki uchumi wao uzidi kuwa mkubwa.

Na sisi TIC tunaendeleza maono ya Rais kwa kuwaunganisha watanzania na wagenii kwa lengo la kushirikiana kwa pamoja na kuwekeza pamoja ili kuleta faida kwa watanzania na chi kwa ujumla.” Ameeleza Teri

Kwa Upande wa Balozi wa Tanzania nchini China, Khamis Mussa Omar amesema kuwa Wachina hao wamekuja kujionea maeneo ambayo wanaweza kuja kuwekeza hasa katika Viwanda vya usindikaji wa mazao ya chakula ambapo hapa nchini tumekuwa tukizungumzia mazao ya biashara, wenzetu hawazungumzii mazao ya biashara wananzungumzia mazao ya Viwanda.
Pia amesema kuwa wamekuja kuangalia uwekezaji wa madini kwaajili ya kuchakata na Kwenda kwenye viwanda.

Mkuu wa Huduma za uwekezaji kutoka Sekta binafsi Tanzania (TPSF), Kinanasi Seif, amesema kuwa wamewaunganisha wafanyabiashara wa nchini na wageni ili waweze kuwekeza pamoja kwaajili ya kuiga teknoloji wanazozitumia katika viwanda hasa katika sekta ya Viwanda, kilimo na Ujenzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini China, Khamis Mussa Omar wakati wa Kongamano la Wawekezaji na Wafanyabiashara lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2024.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad