JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


e-GA yajipanga kuongeza ubunifu katika mifumo ya TEHAMA ya Taasisi za Umma

Share This
Meneja Mawasiliano wa eGA Subira Kaswaga akizungumza na Waandishi wa Habari katika Banda la eGA kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


*Yaunganisha Taasisi 148 katika Mfumo Mkuu wa Ubadilishanaji taarifa  Serikalini (GoVESB)

Na Mwandishi Wetu.
MAMLAKA ya Serikali Mtandao(e-GA), imeahidi kuendelea kufanya tafiti na bunifu za mifumo ya TEHAMA itakayorahisisha upatikanaji wa huduma za Serikali kwa wananchi kidijiti.

Hayo aliyasema Meneja Mawasiliano wa e-GA Bi. Subira Kaswaga, kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, hadi sasa e-Ga imeunganisha taasisi za umma 148 katika mfumo wa GoVESB ambapo mifmo 141 tayari imekwishaunganoshwa  na mifumo 108 ya taasisi 89 inawasiliana na kubadilishana taarifa.

Amesema sasa mfumo ambao unakwenda kutoa suluhisho ni mfumo wa MREJESHO ambao wwananchi akifanya huduma atapataa taarifa moja kwa moja.

Amesema  ndani ya mifumo ya 141  kunapatikana mifumo 148 na kati ya hiyo mifumo 109 inasomana na kupeana taarifa moja kwa na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakati.

Kaswaga amesema kuwa Wakala huo umeanzishwa kwa sheria namba 10 ya mwaka 2019 ikiwa na jukumu kubwa la msingi ni kuratibu matumizi ya Tehema katika taasisi za Umma  kuhakikisha huduma za Serikali zinawafikia wananchi wa mijini na vijijini kwa njia ya kidijiti mahali walipo bila kuangalia mipaka ya mazingira wanayozungukwa.

Amesema mfumo huo ni daraja kati ya taasisi za Serikali na wananchi katika kuwasilisha changamoto na maoni yao mfumo huo umetambulika kimataifa kama ni jukwaa huru linalowasaidia wananchi kupata taarifa za serikali kwa wakati.

Aidha amefafanua kuwa  mifumo  imeweza na kupata tuzo katika Umoja wa Mataifa wa ubunifu wa huduma za umma mwaka 2024 zilizotolewa nchini Korea.

“Mifumo hiyo yote inatumika tunafanya jitihada mbalimbali ikiwa na pamoja na kukutana na taasisi za umma ambapo Julai 22 hadi 29 tunatarajia kukutana na taasisi zaidi ya70 za umma kwa lengo la kuwapa elimu kuhusiana na mfumo GoVESB” amesema.

Amesema taasisi zimekuwa na muitikio mzuri kadiri wanavyoangalia takwimu idadi ya taasisi zinaongezeka na idadi ya mifumo inayounganishwa katika mfumo huo inayobadilishana taarifa inazidi kuongezeka.

“Jukumu letu ni kuhakikisha taasisi zote za umma zinaunganishwa katika mfumo huu ili kubadilishana taarifa”. amesema Kaswaga

Aidha ameongeza kuwa, e-GA kupitia Kituo chake cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa ya Serikali Mtandao (eGOVRIDC),  kimebuni mifumo mbalimbali ya Tehama ambayo italeta tija kwa serikali katika kurahisisha utendaji kazi na itasaidia utoaji wa huduma kwa wananchi kwa njia ya kidijiti.

Kaswaga ametoa wito kwa taasisi za umma na wananchi kuwasilisha maoni na kero kupitia mfumo wa e-Mrejesho pamoja kufika kwa wingi katika ofisi husika kupata elimu zaidi kuhusiana na mifumo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad