Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri kushoto akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 18, 2024 mara baada ya kujionea eneo la Uwekezaji lililopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 18, 2024 alipowakaribisha watendaji wa TIC, TRC na wa wilaya ya Kisarawe kwaajili ya kujione eneo la Uwekezaji lililopo katika wilaya yake.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania(TRC), Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea eneo la Uwekezaji lililopo katika Wilaya ya KJisarawe Mkoani Pwani.
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kitaweka kambi katika eneo la Wawekezaji lililopo Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani pia watatengeneza taarifa za maeneo ya Uwekezaji na kuyapigia debe kwa Wawekezaji wa nchini na Nje ya nchi.
Hayo ameyasema, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri leo Julai 18, 2024 Wilayani Kisarawe walipokaribishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Petro Magoti ili wajioneee maeneo ya Uwekezaji yaliyopo katika eneo lake. Amesema kuwa maeneo hayo yanathamani kubwa nao TIC watayawekea thamani inayostahili.
Teri amesema kuwa maendeleo yatakayopatikana katika maeneo hayo ya Uwekezaji ni kwaajili ya Wananchi wa Wilaya hiyo na wao waanze kufurahia matunda ambayo Rais Dkt. Samia anataka awape wanakisarawe.
Awali akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Magoti, Teri amesema kuwa wilaya hiyo itakuwa sehemu ya msingi na muhimu ya Uwekezaji katika Ukanda wa Afrika Mashariki, itakuwa rahisi kufikika kuliko wilaya nyingine za mkoa wa Pwani kulingana na Jiografia ya eneo hilo pamoja na mipango iliyopo.
Amesema wilaya ya Kisarawe ipo karibu na bandari ya Dar es Salaam Kwa Kilomita 24 na ukaribu wake na Reli ya Mwendokasi ya (SGR) ambapo ipo kilomita 8 tuu lakini pia wana eneo ambalo lipo tayari na limelipwa.
"Ni wazi mwekezaji anayetaka kuwekeza sehemu ya kwanza kuja ni Kisarawe."
Awali akimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Teri amesema, "Namshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti kwa kutuita na kutualika wilayani kwake na kutushirikisha maeneo yake yanayohusu Masuala ya Uwekezaji katika Wilaya nzima ya Kirasawe ni hatua kubwa na nikupongeze sana."
"Ni Moja ya Wakuu wa wilaya wachache ambao wamepiga hatua kutuita sisi Viongozi wa Serikali wa Kisekta kuja kushirikiana moja kwa Moja.
Kwangu ni mara ya Kwanza kuitwa na Mkuu wa Wilaya kuja kuzungumza masuala haya ya Uwekezaji kwahiyo niwapongeze sana." Amesema Teri ikiwa ametimiza mwaka mmoja na nusu katika nafasi yake TIC.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti aliwakaribisha Watendaji wa TIC na TRC ili kuyafanyia kazi maono yake katika masuala ya Uwekezaji wilayani Kisarawe.
Dc Magoti amesema kuwa mji unahamia wilaya ya Kisarawe kwani miundombinu ya kimkakati imepita wilayani mwake na pia barabara ya mwendokasi ikifika Gongo la Mboto basi kwa msafiri atatumia dakika 30 tuu kufika wilaya ya Kisarawe katika maeneo yaliyotengwa kwaajili ya Wawekezaji.
Wakati huo huo DC, Magoti ameonya matapeli waounua maeneo kwa wananchi kwa gharama ndogo ili kufanya udalali pia amewaasa wananchi kutokuuza maeneo hayo ili washirikiane na serikali kuyafanyia kazi.
"Sasa nimeona tuweke wawekezaji katika eneo hili... tunaomba mtuwekee Stesheni ndogo kutokana na eneo hilo kuwa na viwanda vingi ili iwe rahisi kusafirisha bidhaa ndani ya nchi na nje ya nchi." Amesema DC Magoti
Amesema kukiwa na miundombinu katika eneo hilo Wananchi wa Kisarawe watanufaika, foleni itapungua katika jijini la Dar es Salaam lakini kusafirisha mzigo kutoka eneo la Wawekezaji hadi kibaha kwa kupitia Kisarawe ni Kilomita 11 tu na hiyo itasaidia kupunguza mzunguko.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amempongeza RC, Magoti kwa kuwa na maono makubwa kwaajili ya wananchi wake.
"Umefanya jambo kubwa DC Magoti kwaajili ya wananchi wa Kisarawe.....Maeneo ilikopita Reli ni maeneo sahihi ya kuweka Viwanda."
Amesema eneo la Uwekezaji la Kisarawe limepitiwa na SGR hiyo itakuwa rahisi kusafirisha mizigo ndani ya Nchi na Nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kisarawe, Khalifan Sika amewashukuru watendaji wa Serikali kwa kufika katika wilaya ya Kisarawe na Kusimamia maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kusaidia wananchi.
Ziara ya kutembelea wilaya ya Kisarawe ilihusisha Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na Wafanyakazi na Watendaji wa Mamlaka na Taasisi mbalimbali za Serikali za Wilaya ya Kisarawe.
Viongozi mbalimbali wakipewa maelezo kuhusiana eneo la Uwekezaji luiililopo Wilaya ya Kisarawe.
Picha ya Pamoja.
Reli ya Mwendokasi ikipita karibu na eneo la Uwekezaji lililopo Wilaya ya Kisaeawe mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment