Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Nhayalina akimuonyesha eneo lililovamiwa na raia wa Burundi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) wakati wa ziara ya kukagua Mpaka wa Manyovu unaotenganisha nchi ya Tanzania na Burundi.Wengine ni ujumbe ulioongozana na Waziri Masauni katika ziara hiyo mkoani Kigoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Mwandishi Wetu,Manyovu
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ametoa mwezi mmoja kwa Idara ya Uhamiaji nchini kuhakikisha Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mipaka kufanya kazi katika Kituo cha Uhamiaji Manyovu ili kuepusha upotevu wa mapato ya nchi,kuepusha mifumo ya rushwa na kudhibiti uingiaji wa watu wanaoweza kuhatarisha amani ya nchi……
Ametoa kauli hiyo baada ya kukagua shughuli za uingiaji na utokaji wa raia na wageni wanaokwenda nchini Burundi kupitia Kituo cha Uhamiaji Manyovu kilichopo katika Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambapo pia amewataka kuhakikisha wanadhibiti vipenyo mbalimbali vinavyopatikana katika mpaka huo.
‘Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama na hilo ameshalitekeleza na mtaona jinsi alivyowapandisha vyeo askari wa ngazi mbalimbali lakini sasa wajibu uenda sambamba na haki kwahiyo lazima muongeze jitihada katika kufanya kazi zenu,haiwezekani Waziri ndio aje hapa kufuatilia suala la mfumo,mara sijui mfumo wa kiyoyozi aufanyi kazi,sasa nishamuelekeza Kamishna Jenerali kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja mfumo huo unafanya kazi,haiwezekani serikali imewekeza fedha nyingi katika mfumo huu wa uhamiaji mtandao sasa haiwezekani leo usiwe unafanya kazi mnakaa kubeba fedha za wananchi na kuzipeleka benki kwa njia ya kawaida’ alisema Waziri Masauni
No comments:
Post a Comment