JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Serikali Kuzingatia Mikataba wa Hali Bora kwa Mabahari

Share This

 

Naibu Waziri wa Uchukuzi Daniel Kihenzile akizungumza katika Kilele chA Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani na Tanzania yalifanyika wilayani
Katibu wa Vijana wa Chama cha Mabaharia Ally Mzee akisoma lisala kwa mgeni Rasmi kuhusiana na Siku ya Mabaharia Duniani ambayo Tanzania imefanyika wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mohamed Salum akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Bagamoyo mkoani Pwani.


*TASAC yaweka mikakati ya  mifumo ya Kidijitali kwa Mabaharia

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV 
SERIKALI imesema imeendelea kuzingatia hali bora ya use ll Mabaharia chini ya Mkataba wa Kazi za Mabaharia (Maritime Labour Convention 2006 (MLC 2006)) wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambao Tanzania imeridhia. 

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Uchukuzi  Daniel Kihenzile kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Uchukuzi Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakati kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani ambayo huadhimishwa Juni 25 na Tanzania Maadhimisho hayo yamefanyika wilayania Bagamoyo mkoani Pwani,Kihenzile amesema kuwa kwa kuzingatia kupata Mabaharia mahiri Tanzania kupitia Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Serikali  imeendelea kutekeleza matakwa ya Mkataba wa Kimataifa wa viwango vya mafunzo, utoaji vyeti na utendaji kazi wa Mabaharia (STCW - 78).

Amesema kuwa  wataalam wameendelea kujengewa uwezo katika mafunzo mbalimbali ya ndani na ya kimataifa ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi

Amesema kuwa  Shirika la Bahari Duniani (International Maritime Organisation  IMO) lilitenga siku maalum ili kuenzi na kutambua mchango adhimu wa mabaharia ambao ni kiungo muhimu katika uchukuzi kwa Taifa na Dunia kwa ujumla na kuazimia kufanya maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani (Seafarers Day), ambapo, ilianzishwa mwaka 2010 kwa azimio lililopitishwa katika mkutano wa kidiplomasia huko Manila kwa lengo la kuhimiza Serikali na Kampuni za meli kukuza biashara hii ya usafirishaji. 

Kihenzile amesema  Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi mwanachama wa IMO ilijiunga mwaka 1974 na kila mwaka imekuwa ikishiriki katika kuadhimisha siku ya Mabaharia Kitaifa na mwaka huu 
Maadhimisho hayo m yamebeba Kauli mbiu inayosema “Navigating the Future: Safety First kwa tafsiri isiyo rasmi ni Mustakabali wa Uendeshaji Vyombo vya Usafiri Majini: Usalama Kwanza ambapo kauli mbiu hiyo imelenga kuimarisha ulinzi, usalama sanjari na utunzaji wa mazingira endelevu ya Bahari, huku ikihakikisha mchakato wake wa maendeleo ya udhibiti unakuwa kwa kasi kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia na uvumbuzi. 

Aidha vyombo vya Usafiri Majini pamoja na kazi kubwa vinayofanya ya kubeba bidhaa kutoka eneo moja kwenda jingine, pia huchukua taka mbalimbali zinazozalishwa wakati wa safari, na vilevile maji yanayobebwa na meli kwa ajili ya mizania ya meli baadhi ya taka hizo zinakuwa hatari kwa bayoanuai na jamii zinazotegemea rasilimali za majini kukuza uchumi na viumbe wengine. 

"Kwa muktadha wa IMO iliandaa Mkataba wa kuzuia uchafuzi wa mazingira kwa uchafu unaotokana na meli (International Convetion for the prevention of Pollution from ships MARPOL Convention -1997) ambapo   mkataba huo una viambatisho sita (Annexes) hadi sasa Nchi imesharidhia viambatisho vitano, na kwa sasa Wizara iko katika hatua za mwisho za kuridhia kipengele cha sita kinachohusu kuzuia uchafuzi wa hewa kutokana na gesi sumu ya moshi unaozalishwa na meli. Kwa kuridhia Mkataba huo, nchi inawajibika kuzingatia uendeshaji salama wa vyombo ili kuhakikisha tunakuwa na bahari safi na endelevu (Cleaner Oceans and Safer Seas) kwa vizazi vijavyo. 

Amesema usafirishaji kwa njia ya maji umeweza kufanikisha ukuaji wa biashara kufikia asilimia (90) Duniani kote. Bidhaa nyingi husafirishwa kwa meli kutoka bara au taifa moja hadi jingine. Kwa kiwango kikubwa na kwa gharama nafuu. Hivyo, kufanya bidhaa kufika popote duniani na kwa gharama nafuu. Uimarishwaji wa ulinzi na usalama katika sekta hii ni jambo muhimu, kuziwezesha meli kupunguza gharama kubwa za uendeshaji zikiwemo (gharama za bima) zinazoweza kusababisha gharama za usafirishaji kupanda na kuathiri uchumi wa nchi. 

Hata hivyo amesema katika kuadhimisha Siku ya Mabaharia Duniani ni kutambua mchango wa mabaharia katika kuimarisha uchumi wa mataifa na mtu mmoja mmoja. 

Kihenzile ametoa wito kwa  mamlaka na taasisi zenye kutekeleza majukumu yenye mnasaba na mabaharia, kuzingatia kazi za staha na mazingira salama kwa mabaharia. Kufuatilia na kutambua changamoto zinazowakabili mabaharia; kujadili na kuzipatia masuluhisho ili kuwapa furaha wanapoendelea kutekeleza majukumu yao wawapo katika maeneo ya kazi.


"Ni imani kubwa kuwa elimu iliyotolewa itaendelea kutukumbusha kuongeza umakini tunapokuwa katika kutekeleza majukumu yetu kwa lengo la kuondokana na dhana mbaya iliyojengeka kwa baadhi ya watu kutekeleza majukumu kwa mazoea na tabia hiyo imekuwa ikiligharimu taifa kwa kusababisha kuondokewa na nguvu kazi kutokana na majanga na ajali yanayoweza kuzuilika"amesema 

 Amesema wataalamu kujenga hali ya kujifunza zaidi na kutumika kwa weledi, ili kuwa chachu ya mafanikio kwa vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika Sekta ya Usafiri Majini. 

Kihenzile amesema Ubaharia una historia ndefu ambayo imekuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, tukianza kujikumbusha historia ya ”safina  enzi za Nuhu na nchini  kadhalika usafiri huu umetumika kwa muda mrefu hadi kufikia sasa ni maboresho mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika kwenye vyombo na mifumo ya usafiri majini kwa lengo la kuimarisha usalama na mazingira na huduma bora kwa mabaharia na kukua kwa teknolojia na matukio mbalimbali ya ajali za meli vimesababisha kufikiwa kwa maboresho hayo.

Kihenzile amesema  vyombo vikubwa na vidogo kuzingatia taarifa za mara kwa mara za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) pindi wanapojipanga na safari za majini ili kupunguza athari za majanga majini.

"Tumekuwa tukisikia taarifa za vyombo kupoteza mwelekeo majini na ajali kutokana na kukumbwa na hali mbaya ya hewa. Taarifa hizi zitawapa uhakika wa wakati sahihi wa kuingia majini na kwa salama"amesema Kihenzile

Amesema  Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imeendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kielelezo ambapo ikikamilika itaongeza fursa za ajira kwa mabaharia, miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa meli mpya ya “MV. Mwanza Hapa Kazi Tu katika Ziwa Victoria; ujenzi wa karakana ya kujengea meli (shipyard) katika Ziwa Tanganyika;

Ujenzi wa meli ya kubeba mizigo (Ro-Ro & Wagon Ferry) katika Ziwa Tanganyika itakayokuwa na uwezo wa kubeba jumla ya tani 3,500 za mizigo:  malori marefu 25 (long vehicles) au mabehewa 25 ya reli ya kisasa (SGR) katika sakafu ya kwanza (main deck).  Sakafu ya juu (upper deck) itakuwa na uwezo wa kubeba jumla ya magari madogo 65; 

Ujenzi wa meli ya kubeba mizigo (Ro-Ro & Wagon Ferry) katika Ziwa Victoria itakayokuwa na uwezo wa kubeba jumla ya tani 3,000 za mizigo;
Ukarabati wa Meli ya MT Sangara katika Ziwa Tanganyika; 
Ukarabati wa meli ya MV Umoja inayotumika kubeba mabehewa ya reli 22;
Ukarabati wa meli ya MV Liemba katika Ziwa Tanganyika; 
Ukarabati mkubwa wa meli ya kubeba shehena ya mafuta ya  MT Nyangumi iliyoko Ziwa Victoria; 
Ukarabati mkubwa wa meli ya uokozi (Tug Boat) ya MT Ukerewe iliyoko Ziwa Victoria pia imekarabati meli mbili za MV. Victoria Hapa kazi tu na MV. Butiama katika ziwa Victoria ambazo hutumika kusafirsha abiria na mizigo katika visiwa vilivyopo ziwa victoria. 

Amesema  serikali imeshachukua na 
kuridhia kwa mkataba wa Maritime Labour Convention 2006 (MLC 2006), ambao umeweka haki za msingi za Mabaharia, haki hizo ni vipengele vya kulinda maslahi ya Mabaharia, Afya na Mazingira bora ya kufanyia kazi ya Mabaharia, haki ya kurudishwa nyumbani (repatriation, huduma za matibabu (medical assistance), likizo (shore leave), masaa ya kazi na mapumziko, kuweka utaratibu mahususi kwa Mabaharia kuwasilisha malalamiko endapo kama vipengele vya MLC 2006 vinakiukwa. 

Pia mwezi Mei, 2022, kanuni za Maritime Labour Convention zilisainiwa na Waziri wa Uchukuzi wakati huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia ZMA wameingiza Mkataba huo kwenye Sheria yao. Sheria na Kanuni hizo zitakuwa ni msaada mkubwa katika kulinda haki za mabaharia.
 Katibu wa Vijana Chama cha Mabaharia Ally Mzee amesema moja, kuongezeka kwa uelewa miongoni mwa umma kwa ujumla juu ya huduma muhimu za mabaharia zinazotolewa na asasi za kiraia kwa ujumla (ikiwemo Vyama Vya Mabaharia).

Amesema kila baharia  malipo yake ya safari ni tofauti na mwengine, lakini wote wanakabiliwa na changamoto sawa.

 Amesema kauli mbiu ya  Maadhimisho   inaakisi kazi ya IMO ya kuimarisha Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira wa Usafiri wa Majini, huku inahakikisha mchakato wake wa maendeleo ya udhibiti unatarajia kuwa wa kasi kutokana na mabadiliko ya kiteknnolojia na uvumbuzi. 

Mzee amesema 
Nchi yetu kuweza kuridhia mikataba ya kimataifa (22) kati ya Mikataba (59) inayosimamia sheria za Bahari. Ikiwemo, MARPOL 73/78 (Annex I/II), MARPOL 73/78 (Annex III), MARPOL 73/78 (Annex IV), MARPOL 73/78 (Annex V), IMO Convention 48, SOLAS Convention 74, LOAD LINES Convention 66, TONNAGE Convention 69, COLREG  Convention 72, STCW  Convention 78, SAR  Convention 79, IMSO Convention 76, INMARSAT OA 76 nakadhalika.
Mabaharia kuwa na vitambulisho vya kielectroniki.

Ameomba vyuo  vya DMI na FETA kuongeza idadi ya kozi ambazo zilikuwa zinahitajika katika soko la ajira pamoja uwepo wa fursa za kuwajengengea uwezo mabaharia kupitia program zinazotolewa na serekali ya SMT na SMZ, kama vile mikopo ya boti za uvuvi ugavi wa wafanyakazi wa baharini, sio tu kwa meli za kitaifa lakini kwa meli za kigeni
Uimarishaji na ujenzi wa bandari za kisasa nchini kote.

Amesema Mabaharia wa Tanzania wanachangamoto ambazo 
nyenzo dhaifu za kusimamia mambo ya bahari (mbinu zisizo za wazi na zenye kuakisi wakati uliopo) Ukosefu wa sera na kanuni za ajira za ubaharia, (kuwepo kwa mifumo kandamizi za uwajiri wa mabaharia hususan katika makampuni ya ndani) Stahiki duni za mabaharia kama vile; Fidia, Bima, Hifadhi ya jamii na mafunzo kwa vitendo (Sea time).
Mazingira mabovu ya kazi kwa mabaharia na hali zao za kimaisha (hususan kwa vijana na wanawake).

Amesema mambo kadhaa ya kimkakati yakiweza kufanyika kwa juhudi za makusudi ikiwemo tafiti na kakuzi mbali mbali za kina, tutaweza kuibua mambo yafuatayo kutambua idadi kamili ya mabaharia waliopo Tanzania na kujiunga na vyama vya wafanyakazi Kutambua idadi kamili ya Makampuni ya meli yanayoendesha shughuli zake Tanzania yote Kutambua Mabaharia na uwezo wao
Kupata utambulisho mzuri wa vyama kitaifa na kimataifa
Kutumika kwa kazi za kando ya bahari (off shore)

Mzee amesema ajira za mabahria katika meli za kigeni hususan zenye usajili wa bendera ya Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mohamed Salum amesema kuwa wanaanzisha mfumo wa Kidijitali kwa ajili ya Mabaharia  ambapo itasaidia pamoja na kupata leseni.

Amesema wameshaingia mikataba katika nchi 16 kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda kwa ajili ya Mabaharia pale zinapotoka kazi hizo wazipate wakiwa wamekamilika kwa sifa zao.

"TASAC itaendelea kushirikiana na Mabaharia wakati wote pamoja na kushughulikia  changamoto zao"amesema Salum.




Baadhi matukio katika picha katika maadhimisho Siku ya Mabaharia Duniani ambayo huadhimishwa Juni 25 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad