Na Mwandishi Wetu
MKUU wa
Mkoa wa Mwanza Said Mtanda ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa ugatuzi
wa madaraka kwa Kanda zake nchini, kwani uamuazi huo utasaidia na
kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za afya kwa wakati.
Mtanda
ametoa pongezi hizo hapo jana, wakati akifunga kikao kazi baina ya MSD
na Wateja wake wanaohudumiwa na Kanda ya Mwanza ambao ni kutoka mikoa
ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Simiyu na Geita.
Ameeleza licha ya
kuokoa muda wa manunuzi, ugatuzi huo madaraka kwa Kanda, utasaidia
kupunguza mzigo wa majukumu kwa MSD Makao Makuu, na kuleta ufanisi.
Pia
ameipongeza Mènejimenti ya MSD kwa utaratibu wake wa kukutana na wadau
na wateja wake, kujadiliana na kutatua changamoto za upatikanaji wa
bidhaa za afya nchini.
Awali akifungua kikao hicho Mkurugenzi
Mkuu wa MSD Mavere Tukai ameeleza maboresho mbalimbali yanayofanyika
ndani ya Bohari Ili kuleta tija katika kuwahudumia Wateja wake.
Amebainisha
kwamba hivi sasa MSD imewekeza nguvu katika kuboresha maeneo yake ya
Uhifadhi kwa kujenga maghala ya kisasa katika Kanda zake mbalimbali Ili
kuongeza uwezo wa Kanda hizo kuhudumia wateja wake.
Aidha,
amebainisha juu ya mabadiliko na maboresho ya mikataba ya manunuzi hali
iliyopelekea kuongezeka kwa bidhaa ghalani na uwezo wa MSD kukidhi
mahitaji ya Wateja.
Ameongeza kwamba Katika kipindi cha mwaka
2020/21 hadi 2023/24, mapato ya bidhaa za afya yameongezeka kutoka kiasi
cha shilingi bilioni 266 na kufikia takribani shilingi bilioni 530,
Sawa na ongezeko la takribani asilimia 100.
Kwa upande mwingine
Mavere amegusia maboresho ya eneo la huduma kwa Wateja kwa kuimarisha
mawasiliano na mahusiano na wateja, hivyo kuondoa malalamiko na
misuguano isiyo ya lazima.
Naye Meneja wa MSD Kanda ya Mwanza
Bw. Egidius Rwezaura amewashukuru Wadau hao kwa kuitikia wito wa
kuhudhuria kikao hicho, na kuwataka kuendelea kushirikiana Ili kutatua
kwa pamoja changamoto za Upatikanaji wa bidhaa za Afya.




.jpeg)




No comments:
Post a Comment