JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Kutokuwa na Uhakika wa Malipo Chanzo Gharama za Ujenzi wa Miradi- Marwa

Share This
Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Wakandarasi Tanzania (TUCASA) wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Kongamano la Wakandarasi linalofanyika Juni 27, 28, 2024 jijini Dar es Salaam linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Meza Kuu

Na Mwandishi wetu
CHAMA cha Umoja wa Wakandarasi Tanzania (TUCASA), kimesema kutokuwa na uhakika na malipo ndio chanzo cha kuwa na gharama kubwa katika mradi wa ujenzi.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Wakandarasi Tanzania (TUCASA) wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Kongamano la Wakandarasi linalofanyika Juni 27, 28, 2024 jijini Dar es Salaam linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Amesema changamoto hiyo hupelekea Wakandarasi kuweka bei kubwa ya mradi kutokana na kutokuwa na uhakika wa kulipwa, wakati wangekuwa nanauhakika wa kulipwa gharama ingekuwa ndogo.

Changamoto nyingine ni ushiriki mdogo wa Wakandarasi Wazawa kutokana na Miradi mikubwa inayoendelea nchini kufanywa na watu wa nje.

Pia ameiomba serikali kuja na uhakika wa malipo pale kazi inapokuja, kama serikali inakuwa haina fedha kwaajili ya malipo basi benki iwe na uwezo wa kuweka fedha kwaajili ya kuendelea kufanya kazi.

"Kwa kufanya hivyo hakutakuwa na mzigo kwa Wakandarasi, hivyo gharama ya kufanyia kazi itapungua.

Lakini wito wetu kwa serikali tuendelee kuboresha mpaka tufike mahali sisi Wakandarasi wazawa ndio tufanye hizi kazi, tujenge reli, bwawa la Mwalimu Nyerere, Viwanja vya ndege pamoja na Viwanja vya ndege pamoja na madaraja." Ameeleza Marwa

Pia ametoa ushauri kwa serikali ianze kufikilia kulifanyia kazi na mwishowe tufikie kwenye utekelezaji wenye gharama nafuu.

Marwa ametoa wito kwa wadau na kuwaalika wakandarasi wote Tanzania nzima ambao hawajajiunga na TUCASA wajiunge ili wawe na sauti ya pamoja ambayo itawatoa katika changamoto mbalimbali wanazozipitia ili pia Serikali iwe na eneo moja la kuzungumzia pale wanapokuwa na ushirikiano wakandarasi.

Amesema wametengeneza TUCASA kama chombo cha mazungumzo ya pamoja ili kuwawezesha kukutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya pamoja.

Akizungumzia nafasi ya Wakandarasi nchini Marwa amesema kuwa ukiangalia bajeti kuu ya serikali zaidi ya asilimia 60 ya fedha zote inaenda katika miundombinu ambayo wakandarasi ndio watekelezaji wake.

"Sisi ndio tunatekeleza sehemu kubwa ya bajeti ya Serikali."
Meneja TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, Jofrey Mkinga amesema kuwa hakuna TARURA bila wakandarasi kwa sababu ndio wanaoshirikiana katika kutekeleza kazi zao kwa asilimia 99.

"Kwetu sisi TUCASA ni mtu na nduguye kwa maana hatuwezi kuachano, ushirikiano wetu ni wakindugu sisi pamoja na TANROADS


Kwa Upande wa Mshiriki Mwanamke katika Kongamano la TUCASA, Maida Waziri amesema kuwa wamekutana Wakandarasi kwaajili ya kutathimini changamoto na Mafanikio yao, pia mkupongeza Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya hasa kwenye Miundombinu mbalimbali ambayo inafanyika hapa nchini.

Amesema kuwa kongamano hilo pia litasaidia kuwangalia Wakandarasi Wazawa 'Local Content' wanapata kazi na kulipwa kwa wakati.

Amesema wameona kwenye sera na sheria mbalimbali kuna mabadiliko makubwa ambayo yametokea na anaamini kabisa katika mwaka mpya wa serikali unaokuja wameweza kuongezewa bajeti ya serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) na Wakala wa Barabara (TANROADS).



Baadhi ya wakandarasi wakiwa katika Kongamano la wandarasi jijini Dar es Salaam leo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad