WAKALA
wa wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA) wamezitaja ada za usajili wa
kampuni mpya ambapo gharama zake zinaanzia Sh.20,000, Sh.1000,000,
Sh.5,000,000,Sh.20,000,000 mpaka Sh.50,000,000 na kwamba viwango hivyo
ni kutokana na mtaji wa kampuni husika na kwa usajili wa kampuni za
kigeni gharama za usajili ni Dola za Marekani 1,190,Filing fee ni
Sh.66,000 na Stamp Duty 6,200.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo Juni 20,2024 mkoani Morogoro wakati akitoa mada inayohusu usajili
wa Kampuni kwa waandishi wa habari wa biashara wanaoendelea na kujengewa
uwezo kuhusu majukumu ya BRELA ,Mkuu wa Sehemu ya Kampuni kutoka
Kurugenzi ya Kampuni na Majina ya Biashara wa Wakala huo Lameck Nyangi
amesema pamoja na mambo mengine mtu kaunzia mmoja au wa wawili ambao
wanataka kusajili kampuni yao wanatakiwa kuwa na taarifa za msingi
ambazo wanatakiwa kujaza katika fomu.
Amesema ili kusajili
kampuni pia unapaswa uwe na akaunti pamoja na nywila ili kuingia katika
mfumo wa BRELA kufanya usajili na kusisitiza katika usajili huo lazima
kuwepo na taarifa muhimu za wakurugenzi kwa maana ya namba zao za NIDA
na TIN No lakini pia lazima kuwe na adresi kama ni mmoja au zaidi .
“Kama
ni wageni wa nje lazima uwe na hati ya kusafiria lakini lazima kuwepo
na jina la kampuni na jina lenyewe lisifanane na lingine, lisiwe la
matusi. lisiwe na uhusiano na majina ya Serikali.Lakini kubwa katika
kampuni lazima uwe na Katiba pamoja na muongozo au muongozo wa kampuni
Aidha
amesema Sheria ya usajili wa kampuni katika kifungu cha nne mpaka cha
tisa kimeeleza namna gani mkataba wa kampuni au kanuni za uendeshaji
unatakiwa kuandaliwa. Hata hivyo taratibu za usajili wa kampuni , kuna
mabadiliko yaliyotokea ambayo yalisababisha matumizi ya mtandao na BRELA
kuanzia mwaka mwaka 2018 ilitambulisha mfumo wa kusajili kampuni kwa
njia ya mtandao.
Pamoja na hayo Nyangi amesema usajili wa kampuni
unafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni ya Tanzania ya mwaka 2002
ambayo ilikuwa haina tofauti na Sheria ya 1932 ambayo chimbuko lake ni
Sheria ya Kingereza ya mwaka 1929.
“Lakini wengine wanasema
chimbuko halisi la sheria imetokana na kampuni za India mwaka 1913
lakini sheria zote mbili zinamchango mkubwa kwa sheria ya kampuni ya
Tanzania ya mwaka 1932.Kuna mfanano wa vifungu vingi ambavyo vimeletwa
katika sheria ya kampuni nchini Tanzania.
“Baada ya kufika mwaka
1932 tulipoamua kuwa na Sheria za kusimamia kampuni na kuendeleza
kampuni sheria yetu ilione ichukue vifungu vya sheria zile za
Kingereza.Kwa hiyo uhalisia wa chimbuko la Sherie za kampuni imeanza
mwaka 1929 na mwaka 1932 ndio tukaja na sheria ya kampuni sura namba
212.
“Lakini Sheria ya mwaka 1932 ilfutwa na sheria ya mwaka 2002
kwa maana ilitengezwa sheria mpya ya kampuni. Na hivyo kuwa na sheria
mpya na ikabaki na sura ile ile ya 212 lakini sheria hii bahati mbaya
ilipitishwa na Rais na kuanza kutumika mwaka 2006.Kwa hiyo pamoja na
sheria kutungwa katika kipindi cha miaka sita iliendelea kutumika sheria
ya mwaka 1932,”amesema.
Home
Unlabelled
BRELA YAWEKA WAZI VIWANGO VYA ADA USAJILI WA KAMPUNI
BRELA YAWEKA WAZI VIWANGO VYA ADA USAJILI WA KAMPUNI
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
No comments:
Post a Comment