JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


UTT AMIS, VERTEX WATOA ELIMU UMUHIMU WA KUWEKEZA ILI KUJIANDAA NA MAISHA YA KUSTAAFU

Share This

 
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


MIFUKO ya UTT AMIS kwa kushirikiana na Kampuni ya Vertex International Securities Ltd wametoa mafunzo kwa wananchi wa kada mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa Lengo la kuwaelimisha umuhimu wa kuwekeza katika mifuko ya UTT AMIS kwa ajili ya kujiandaa maisha baada ya kustaafu.

Mafunzo hayo yametolewa Mei 4,2024  jijini Dar es salaam ambapo maofisa wa UTT AMIS kwa kushirikiana na Maofisa wa Vertex wameelezea kwa kina Kuhusu umuhimu wa jamii kujenga utaratibu wa kuwekeza katika mifuko hiyo ili kujiandaa na maisha ya kustaafu.

Akizungumza kuhusu semina hiyo Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Daudi Mbaga amesema katika maisha ya kufanya kazi kuna wakati kustaafu ambao unaweza kuwa ukomo kwa mujibu wa Sheria kwa maana ya kustaafu unapofika miaka 55,60 na kwa madaktari na maprofesa miaka 65.

"Wakati mwingine si hivyo tu unaweza kustaafu kabla ya umri huo, kwa mfano Kampuni au Taasisi imefilisika au wakati mwingine unaweza kustaafu kwasababu ya afya,hivyo si lazima ufike wakati wakati huo. Kwa hiyo wakati unaanza kazi ujue siku moja utastaafu, Hivyo kuna haja ya kujiandaa

"UTT AMIS na Vertex tuliona kuna fursa ambazo zipo UTT AMIS ,fursa ambazo ziko katika hatifungani za serikali na fursa kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam.Ni sehemu ambapo kwa kutumia fursa hizo linaweza kuwa suluhisho kwa maisha baada ya kustaafu,"amesema.

Ameongeza kwa hiyo wameona iko haja ya kuandaa semina hiyo na kuita wananchi kutoka kada mbalimbali kwa ajili ya kuwapa elimu hiyo muhimu na kama inavyofahamika mtu akipata elimu anakuwa na weledi kwenye jambo fulani hata kukabiliana nalo."Kwa hiyo ndilo kubwa ambalo limetuleta hapa."

Kuhusu mwitikio ilivyo katika uwekezaji wa mifuko ya namna hiyo katika UTT AMIS amesema Kampuni ya Vertex ni Kampuni inayokuwa kwa kasi kwasababu watu wengi wanashiriki kwenye masoko ya fedha na mitaji.

Amesema kwa upande wa UTT AMIS ametoa mfano kuwa ukiangalia mfuko pendwa wa wastaafu ni mfuko wa Hatifungani ambao una miezi kama 55 au 56 tangu ulipoanzishwa lakini unahudumia idadi kubwa ya wastaafu na una zaidi ya Sh.bilioni 600.

"Pamoja na hayo wastaafu pia wako katika mifuko mingine kwasababu ukija pale UTT unachagua mfuko ambao unataka,kwa hiyo tunaweza kusema mwitikio ni mkubwa na kwasababu tu ya changamoto ambazo wakati mwingine ziko kwenye maeneo mengine ambapo wastaafu wangeweza kuwekeza.

"Unakuta mstaafu amefanya kazi miaka 30 hajawahi kufuga kuku lakini akipata fedha ya kustaafu unaenda kwenye kufuga kuku wanampiga chenga au wakati mwingine hujawahi kumiliki daladala unapoenda kununua daladala kwasababu unahela baada ya muda mfupi unajikuta uko nje ya biashara matokeo yake unapata mfadhaiko au ukapoteza maisha

*Kwa hiyo UTT AMIS imekuwa ni suluhisho na tumekuwa tukitoa mafunzo kila siku na kokote kwenye uihitaji tunakokwenda na tunatoa mafunzo na mafunzo haya ni bure,"amesema na kufafanua kuwa idadi ya wawekezaji katika mifuko hiyo inafikia watu 50,000 licha ya kwamba Tanzania ina watu milioni 60

"Lakini ukumbuke watu ambao wako kwenye ajira rasmi kwa mfano Serikalini na wenyewe wako kwenye 500,000 na mara nyingi ndio unaanza na hawa na kisha unaenda kwa mkulima au kufanya biashara kumuelimisha."

Kwa upande wake Meneja wa Utafiti wa Vertex International Securities Ltd, Bwa. Beatus Mlingi amesema kuwa asilimia kubwa ya Watanzania bado wanawekeza katika njia za kitamaduni kama kilimo, ufugaji na biashara nyingine.

Amefafanua lakini katika hizo bidhaa za kifedha,hisa, hatifungani na vipande vingine bado uhusika wa Watanzania umekuwa mchache ,kwa hiyo hizo semina ambazo wamekuwa wakiziandaa kwa ushirikiano wa UTT AMIS wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi.

"Watu wanaposikia kustaafu wanawaza mtu mzee lakini kustaafu ni pale tu unapoacha kutumia nguvu kazi ili kupata kipato, kwa hiyo unaweza kuwa na miaka 20 lakini tayari unarasilimali ambazo zinakuzalishia ,zinaweza kukulisha ,kukutibu,kukulipia gharama zako za kuishi za siku na siku kwa muda wote uliobaki kwa maisha yako

"Maana yake hapo unaweza kustaafu kwani uhitaji tena kwenda kujiajiri au kuajiriwa au kutafuta njia za kupata kipato kwa kutumia nguvu kazi yako.Huko ndio kustaafu sio mpaka ufike miaka 60.

"Kwahiyo tunaposema tunatoa semina ili watu kutumia mbibu kutengeneza mikakati na kupata mbibu za kuweza kuwekeza kwenye hizi bidhaa za kifedha hasa kwa kupitia huduma zinazotolewa UTT AMIS au huduma zinazotolewa na Vertex ili uweze kustaafu vizuri na haimaanishi kwa wazee peke yake.

"Dhana ya kwamba mstaafu ni mzee imepitwa na wakati kwani unaweza ukastaafu hata ukiwa na miaka 25 ilimradi uwe unarasilimali za kutosha za kuweza kukufanya ukagharamia mahitaji yako ya siku bila wewe kuamka saa mbili mpaka saa 11 ukiwa unatumia nguvu kazi yako kupata kipato kama mshahara au unapoenda kufungua duka."

Kuhusu kutathimini mchango wao katika Soko la Hisa amesema vertex ndio Kampuni muanzilishi katika Soko la Hisa kwani wamekuwa bega kwa bega na sio tu katika mwanzo wa soko la Hisa bali katika ukuaji wake wote.

"Na umeona hivi karibuni tumesaidia kuleta sokoni hatifungani ya TangaUwasa lakini huu ni mchango ambao Vertex tumeutoa,"amesema na kufafanua Kampuni yao ni moja kati ya Kampuni za juu kabisa na kiongozi ambazo zinashughulika na hisa na hatifungani

"Na ushirikiano wetu sisi na UTT AMIS haujaanza leo jana,ni ushirikiano wa muda mrefu.Tukio la leo linadhihirisha ukaribu na ushirikiano mzuri uliopo kwa hiyo ni ushirikiano wa kipekee."


 Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano UTT AMIS  Daudi Mbaga akizungumza wakati wa mafunzo yaliyofanyika Mei 4,2024 kwa wananchi wa kada mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa Lengo la kuwaelimisha umuhimu wa kuwekeza katika mifuko ya UTT AMIS kwa ajili ya kujiandaa maisha baada ya kustaafu.
Meneja wa utafiti wa Vertex International Securities Ltd, Bwa. Beatus Mlingi akifafanua jambo kwa wananchi wa kada mbalimbali walioshiriki mafunzo ya Elimu kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika mifuko ya UTT AMIS kwa ajili ya kujiandaa maisha baada ya kustaafu.
Baadhi ya Washiriki wa kada mbalimbali wakifuatilia  mafunzo yaliyokuwa yakitolewa ukumbini humo, jijini Dar es Salaam kwa Lengo la kuwaelimisha umuhimu wa kuwekeza katika mifuko ya UTT AMIS kwa ajili ya kujiandaa maisha baada ya kustaafu.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad