JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Madaktari bingwa wa Ganzi wakutana kujadili changamoto zao

Share This

 Dkt.Edwin Lugazia Rais wa Madaktari wanaotoa huduma ya dawa ya usingizi na ganzi nchini akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa nane wa chama hicho unaofanyika kwa siku mbili kuanza leo Mei 9, jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mboni Chilale mwanafuzi wa udaktari bingwa wa dawa za usingizi na Ganzi kutoka Muhas akizungumza.
Dkt. Victoria Adonicam kutoka KCMC akizingumza
Katibu wa chama cha Madaktari wataalamu wa dawa za usingizi na ganzi salama Dkt. John Kweyamba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa nane wa chama hicho unaofanyika kwa siku mbili kuanza leo Mei 9, jijini Dar es Salaam.


*Wadai bado kuna upungufu wa wataalamu

Na Karama Kenyunko,Michuzi Tv 
CHAMA cha Madaktari Bingwa wanatoa huduma ya dawa ya usingizi na Ganzi nchini (SATA) wamesema  bado kuna upungufu mkubwa wa wataalamu wanaotoa huduma ya hiyo  hususan katika hospitali za wilaya .

Amesema, Serikali imeweka miundombinu ya kutosha ya usingizi salama ikiwemo mashine za kutosha,  vitendea kazi pamoja na madawa ya kutosha lakini bado wanakabiliwa na chagamoto ya kutokuwa na watoa huduma wenye weledi wa kutosha.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa nane wa chama hicho unaofanyika kwa siku mbili kuanza leo Mei 9, jijini Dar es Salaam Dkt.Edwin Lugazia  Rais wa Madaktari wanaotoa huduma ya dawa ya usingizi na ganzi nchini amesema
jumla ya washiriki 250 wanatarajiwa kuhudhuria ambapo wataweza kujadiliana na kupata mafunzo ya vitendo kwa nadharia na kubadilishanavmawazo.

Amesema, licha ya ongezeko dogo la wataalam kwenye taaluma hiyo lakini sasa kumepatika nuru ukilinganisha na miaka 1990 ambapo wataalam walikuwa watano tu lakoni sasa wamefikia 85 nchi nzima.

"Katika kukabilina na chagamoto hiyo tumekuwa tukiendelea kujengeana uwezo katika aina tofauti za upasuaji ikiwa ni pamoja na namna ya kutoa usingizi salama pamoja na kuwahudumia mahututi  wanaohitaji dawa za usingizi" amesema Dkt. Lugazia

Hata hivyo Dkt. Lugazia amesema wanatarajia hivi karibuni changamoto hito ya wataalamu kumalizika kwani kwa sasa madaktari wanaosomea kuwa mabingwa wa dawa za usingizi walioko vyuoni wakimaliza watafikia idadi ya wataalamu 100 nchini.

“Kwa Sasa Vituo vingi vimeongezwa tunahitaji kukimbizana kufundisha watoa huduma ambao wataweza kutoa huduma hizi kila Mahali ambapo kwa sasa vyuo vinavyotoa huduma hiyo ni pamoja na  Bugando, KCMC  MUHAS," amesema Dkt. Lugazia

“Mkutano huu umekuwa ulifanyika kila mwaka kwa Wanataaluma kwa lengo la kujadiliana na kubadilisha uzoefu sambamba na mafunzo tofauti tofauti pamoja na kujengeana uwezo katika ngazi ya chini mpaka ya juu hadi ya kimataifa”, amesema

 Kwa upande wake Katibu wa chama cha Madaktari wataalamu wa dawa za usingizi na ganzi salama Dkt. John Kweyamba  amesema pamoja na kikao cha kujengeana uwezo lakini kuna fursa kwa madaktari kujifunza zaidi.

" chama hiki kina fursa za kidunia ikiwa mafunzo ya ubobezi zaidi kwa wanachama kwenda kwenye nchi zilizoendelea zilimo kwenye shirikisho la wataalam wa ganzi WSFA chama cha wataalam ganzi na usingizi duniani" amesema Dkt. Kweyamba

“Tunakili kuwa chagamoto zipo lakini Kwa sasa zimepungua kutokana na madaktari bingwa nchini kuongezeka...tumekuwa tukiwajengea uwezo katika mikoa hasa wauguzi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi”amesema Dkt. Kweyamba.

Naye, Dkt. Mboni  Chilale  mwanafunzi wa udaktari bingwa wa Ganzi na Usingizi  chuo kikuu cha Muhimbii (Muhas) amaesema anategemea kupata vitu vikubwa kuhusu eneo hilo la utabibu wa usingizi na Ganzi.

Amesema kuwa namna bora ya kumuhudumia mgonjwa vizuri inaanza wodini kabla ya kuingizwa kwenye chumba cha upasuaji.

Dkt . Victoria Adonicam kutoka KCMC  amesema kuwa wataalam wa ganzi na usingizi wamekutana kujadili namna bora ya utoaji ganzi salama pamoja na changamoto.

Amesema kuwa lengo na mkutano huo ni kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ganzi salama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad