JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WADAU WAOMBA WANAWAKE MAULAMA WAWE SEHEMU YA MAAMUZI

Share This

Na Nihifadhi Issa Zanzibar.
SHERIA ya Ofisi ya Mufti wa Zanzibar ya mwaka 2021 kwenye kipengele cha ufafanuzi imefafanua Ulamaa kuwa ni “ Mwanachuoni wa Kiislamu mwenye elimu ya kutosha ya fani mbalimbali ya dini ya kiislam na lugha ya kiarab”. Hapana hakuna sehemu iiyowekwa jinsia maana wanawake na wanaume wenye uwezo wa kielimu wapewe nafasi. Ila suala hili kwa baadhi ya dini ni jambo lisilopewa kipaombele.

Sheikh Khamis Shabaan Khamis ni Iman wa Msikiti pia ni Kiongozi wa dini anayepinga suala la wanaume kuona na kuzungumza kuwa wanawake hawana haki ya kuwa kwenye sehemu za maamuzi, amesema suala la kuharamisha na kuhalilisha suala lolote la kidini ni jambo ambalo linatakiwa litokane na Quran na Mafundisho ya Mtume Muhammad (S.W.A).”Kumzuia mwanamke asishiriki katika utowaji wa Fatwa au maamuzi, kumharimisha wanamke asishiriki katika harakati za kijamii au kutokuwa kadhi au kiongozi basi lazima awe na Ushahidi.” Sheikh Khamis amesema maana yake ni kwamba hakuna pingamizi ya wanamke kuwa kiongozi au kuwepo kwa masuala ya kusema hili halifai.

Dkt Mzuri Issa ni Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar – TAMWA-Z amekuwa akizungumzia suala la usawa na ushirikishwaji wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi anasema .”Kikatiba wanawake wanahaki ya kuwa kwenye sehemu za maamuzi, ni ukweli usioficha kuwa wanawake wanakuwa huru kuzungumza na wanawake wenzao kuliko wanaume hususan kwenye matatizo kama hayo ambayo yanayowakumba zaidi wanawake “Dkt Mzuri anaendelea kusema kuwa kukosekana kwa wanawake kwenye sehemu za maamuzi inaweza kuwa wanawake hawaridhiki na maamuzi yanayotolewa “Ikiwa wanawake wanakosekana kwenye vyombo vya maamuzi ambavyo vinawajibika kwenye masuala haki basi hapo hakuna utekelezaji wa haki,wala usawa na inawavunja moyo sawa wanawake waliosomo kwenye kada hizo wakikosa nafasi za kushirikishwa au kupatiwa nafasi naweza kusema hawatendewi haki” Amemalizia Dkt Mzuri Issa.

Amina Salum Khalfan ni Mwanarakati wa Kiislam anapingana na mawazo ya viongozi wa dini wasioamini nafasi ya mwanamke kwenye masuala ya kijamii na upatikanaji wa haki. “Nikiletewa kesi nawaambia nendani ofisi ya Kadhi au ya Mufti wanawake wanakataa kwa sasa huwezi kuzungumza faragha zako za ndani zinamhusu mwanaume mbele ya wananaume wenzao ni aibu na sio jambo linakubalika kidini “Anaendelea kusema “Kuna madhara makubwa ikiwa wanawake hawatapata nafasi kwenye sehemu hizo maana dini haijasema hivyo, wanaona uzito kwenye suala hili maana waliowengi wameshikilia dini na kukosa maarifa ya hio dini lakini zaidi ni mitazamo yao” Amemalizia kusema Amina.

Mwaka 2019 kupitia Baraza la Wakilishi kulizuka mjadala mkubwa juu ya suala la wanawake kupatiwa nafasi kwenye sehemu za maamuzi huku baadhi ya wawakilishi wakipinga suala hilo kwa kunasabisha dini kukataza baadhi ya masuala ya wanawake kuwa hawafai kuwa kwenye baraza la Maulama .Novemba 27, 2019 kupitia kikao cha kwanza,Mkutano wa 16 wakati wa kuwasilisha Mswada wa Marekebisho ya Kuanzishwa Afisi ya Mufti Nam.9 ya Mwaka 2001 ambao kupitia kikao hicho wajumbe wa Baraza la Wakilishi walijadili kuhusu nafasi ya kuwepo wa maulamaa wanawake.

Akichangia muswada huo Rashid Makame Shamsi ambaye alikuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni alihoji juu ya kuwepo kwa wajumbe 16 wanaume katika baraza la Maulama “Sasa Wajumbe waliotajwa katika Baraza hilo ukipiga mahesabu ni wajumbe 16, sasa ndani ya Wajumbe 16 ni Masheikh, Shekhe mmoja mmoja kutoka kila wilaya na wilaya tuna 10. Sasa ukitizama sitarajii kwamba ndani ya hao Masheikh watakuwemo Masheikh wanawake sitarajii. Kwa sababu ulamaa ni mtu mwenye elimu ya juu katika uwanja wa dini kwa mujibu wa kamusi zote za kiswahili na watu wenye upeo wa dini ya kiislamu wanawake hivi sasa wako wengi sana na kazi kubwa sio kutoa fatwa ni kumshauri Mufti wa Zanzibar.Mimi sifikirii kabisa na nimefanya utafiti kwa Masheikh maulamaa na wasomi wa dini ya kiislam suala hili halina madhara kuwaingiza wanazuoni wanawake katika Baraza la Maulamaa la Zanzibar” Alimalizia Rashid Makame Shamsi – Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni- Zanzibar.

Kupitia Hansad za Baraza la Wakilishi Zanzibar aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Mwalimu akijibu hoja na wajumbe waliochgia mjadala huo aliunga mkono hoja ya kufanyika kwa marekebisho ya baadhi ya vifungu hivyo na wanawake wapate nafasi ya kuingia kwenye Baraza ma Ulamaa kupitia Afisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar “hili la uanzishwaji wa Baraza la Ulamaa, sisi binafsi ushauri huu ulitolewa awali kuona uwezekano pengine na akina mama waweze kuwemo katika Baraza hili.Lakini vile vile, tuangalie uwezekano kwamba kina mama wanaweza kwamba hapa wasiorodheshwe kwamba wawepo katika hii sheria na mimi naungana nao moja kwa moja kwamba ziwepo pengine nafasi mbili za kina mama za wanawake katika Baraza hili.” Alimalizia kuchangia hoja hio.

Jamila Mahmoud ni Mkurugenzi wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Zanzibar – ZAFELA amesema suala la kuwepo kwa msisitizo wa kuchaguliwa na kupatiwa nafasi kwa Maulama wanawake halipo kisheria hivyo hio ni miongoni kwa sababu kubwa ya wanaotoa nafasi cha kuchagu kuona hili jambo sio lazima na halina umuhimu “ Kwa mfano Sheria ya Mahakama ya Kadhi yam waka 2003 Kifungu cha 10(4) “Sheri ya Ofisi ya Mufti wa Zanzibar yam waka 2021 kwenye kipengele cha ufafanuzi imefafanua Ulamaa kuwa ni “ Mwanachuoni wa Kiislamu mwenye elimu ya kutosha ya fani mbalimbali ya dini ya kiislam na lugha ya kiarab”. Hapana hakuna sehemu iiyowekwa jinsia maana wanawake na wanaume wenye uwezo wa kielimu wapewe nafasi.

Jamila ameongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo kwenye suala la wanawake Maulama kutokuwepo kwenye ngazi za maamuzi ni kwa sababu wanaopata nafasi za kuwateuwa hao maulama bado wanaamini kwenye mifumo dume”. Amemalizia Jamila.

Ofisi ya Mufti Mkuu kutokuwateua wanawake kwenye baraza la Maulamana Sheikh Khalid Ali Mfaume ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar amesema wao hawana jukumu la kuwapatia wanawake nafasi ila Serikali ndio inajukumu hilo na pia serikali inazingatia vigezo maalum vya kupewa ajira. “Wanawake wanamchango wao kwenye jamii ila bado suala la wanawake kuwa kwenye baraza la ulama ani suala ambalo linahitajika kufanyiwa kazi” Alimalizia Sheikh Khalid.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad