LIGI ya mabingwa ulaya hatua
ya nusu fainali kurindima wiki hii ambapo miamba minne ya soka itacheza michezo
yao ili kujikatia tiketi ya kufuzu fainali ya michuano hiyo itakayopigwa katika
dimba la Wembley nchini Uingereza.
Vilabu hivo vinne vitakavyokua vinawania tiketi ya kwenda
Wembley ni Bayern Munich kutoka nchini Ujerumani ambao wao leo watakipiga na
Real Madrid katika nusu fainali ya kwanza, Huku ndugu zao kutoka Ujerumani
klabu ya Borussia Dortmund wao watakipiga dhidi ya mabingwa wa Ufaransa klabu
ya PSG katika nusu fainali ya pili kesho Jumatano.
Nusu fainali ya kwanza leo ambayo itawakutanisha miamba ya
soka barani humo klabu ya Bayern Munich bingwa mara sita wa michuano hiyo
akicheza na Real Madrid bingwa mara kumi na nne wa michuano hiyo, Unatarajiwa
kua mchezo mkali kutokana na ubora wa vilabu hivo.
Mchezo kati ya Bayern Munich na Real Madrid ni mchezo wenye
hadi kubwa sana barani ulaya mara nyingi wanapenda kuuita European Clasico kwa
maana vinakutana vilabu ambavyo vina historia kubwa kwenye michuano hiyo
mikubwa kabisa barani humo.
Vilabu hivo vimekutana mara 26 kwenye michuano ya ligi ya
mabingwa barani ulaya ambapo klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kushinda mara
12, Huku Real Madrid wakishinda mara 11 na mchezo
huo ukimalizika kwa sare mara 3, Bayern Munich wakifunga mabao 41 Real Madrid
wao wakifunga mabao 39.
Suka mkeka wako kwenye michezo mikali ya ligi ya mabingwa
ulaya hatua ya nusu fainali itakayopigwa leo Jumanne na kesho Jumatano. Machaguo
zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini
sasa? Ingia meridianbet na
ubashiri sasa.`
Mchezo mwingine wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani
ulaya ambao utarindima ni kati ya klabu
ya Borussia Dortmund dhidi ya klabu ya PSG kutoka kule nchini Ufaransa ni
mchezo ambao pia unatazamiwa kua na uhsindani mkubwa, Kwani vilabu hivyo vyote
vimeonesha ubora mkubwa mpaka kufikia hatua hii.
Borussia Dortmund wamefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali
baada ya kuwapa kipigo cha kushangaza klabu ya Atletico Madrid, Kwani mchezo wa
kwanza Atletico walipata matokeo ya ushindi wakiwa nyumbani mabao mawili kwa
moja lakini Dortmund walipindua meza wakiwa katika dimba la nyumbani na
kushinda kwa mabao manne kwa mawili.
PSG wao stori yao inafanana na ya wapinzani wao Dortmund kwani
mchezo wa kwanza walipoteza nyumbani kwa mabao mawili kwa moja mbele ya Barca,
Lakini walienda ugenini na kufanikiwa kupindua meza na kupata ushindi wa mabao
manne kwa moja na kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali.
Vilabu hivi vimefanikiwa kukutana mara nne tu kwenye michuano
ya ligi ya mabingwa ulaya ambapo klabu ya Borussia Dortmund wakipata ushindi
mara moja, Huku klabu ya PSG wao wakipata ushindi mara mbili na mchezo huo
ukimalizika kwa sare mara moja.
No comments:
Post a Comment