Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Nchimbi amesema ataongeza msukumo kwa serikali kuhakikisha mradi wa Barabara ya Stalike - Kibaoni unaendelea na kukamilika kwa wakati kutokana ili kumaliza kilio cha wananchi wa Katavi cha uhitaji wa barabara kwa kiwango cha lami katika eneo hilo.
Ameyasema hayo leo asubuhi, aliposimama kuwasalimia wananchi wa Kata ya Kibaoni, Halmashauri ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi akiwa njiani kuelekea Mkoani Rukwa, kuendelea na ziara yake kwa mikoa 6 ya Nyanda za Juu Kusini.
Akizungumza na wananchi hao, Balozi Dk Nchimbi amewasilisha salamu za upendo za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Balozi Dk Nchimbi ametoa pongezi kwa wabunge wote wa Mkoa wa Katavi kwa jinsi wanavyoshirikiana na Chama na Serikali katika utekelezaji wa Ilani unaoendelea vizuri na sasa umefikia zaidi ya asilimia 90.
Vilevile, amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa kazi kubwa ya kilimo wanayoifanya na kuwa mojawapo ya mikoa inayozalisha chakula kwa wingi nchini.
NCHIMBI: TUTAWEKA MSUKUMO KILIO CHA LAMI KIBAONI, KATAVI
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
No comments:
Post a Comment