Aliyekuwa msajili wa Mahakama Kuu Tanzania, Jaji Wilbert Chuma (kulia) akikata utepe kama ishara ya kukabidhi ofisi kwa Msajili Mkuu wa Mahakama hiyo mpya nchini, Eva Nkya..anayeshuhudia nyuma ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabrieli. Hafla za makabidhiano hayo zimefanyika leo Aprili 18,2024 jijini Dar es Salaam.
Msajili Mkuu mpyw wa Mahakama Kuu Tanzania, Eva Nkya akizungumza wakati wa kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa msajili wa Mahakama hiyo nchini Jaji Wilbert Chuma (kushoto) kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Profesa Elisante Ole Gabrieli.
Aliyekuwa msajili wa Mahakama Kuu Tanzania, Jaji Wilbert Chuma (katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi ofisi kwa Msajili Mkuu wa Mahakama hiyo mpya nchini, Eva Nkya (aliyeko kushoto na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Profesa Elisante Ole Gabrieli
MSAJILI Mkuu wa Mahakama nchini Tanzania Eva Nkya amekabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Msajili wa Mahakama hiyo Jaji Wilbert Chuma huku mbele yake yamkabili majukumu 12.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 18 Aprili 2024, jijini Dar es Salaam katika Msajili Mkuu wa zamani (Chuma) na Msajili Mkuu mpya (Nkya).
Jaji Chuma wakati anamkabidhi Ofisi kwa Msajili Mkuu alimpitisha kwenye kifungu cha Sheria ya usimamizi wa Mahakama Na. 4 ya 2011.
"Kama mnavyofahamu, kwa mujibu wa kifungu 28 cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na.4/2011 shughuli zote za kimahakama zinasimamiwa na Msajili Mkuu. Msajili Mkuu ndiye kiungo kwa masuala yote ya Sheria kati ya Mahakama ya Tanzania na Mihimili mingine ya Dola pamoja na Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na Mashirika binafsi" amesema Jaji Chuma.
Amesema kuwa majukumu ya msajili yaliyoanishwa kisheria ni pamoja n
Kuwezesha na kusimamia ufanisi katika uendeshaji wa mashauri Mahakamani; Kuratibu shughuli zote za uendeshaji wa mashauri, Kuwa kiunganishi kati ya Mahakama na Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye masuala ya uteuzi, upandishaji madaraja na masuala ya maadili kwa Maafisa Mahakama.
Ameongeza wajibu mwingine ni pamoja na Kuwasiliana na Serikali katika masuala yanahusu mambo ya kimahakama, au masuala yoyote ambayo Serikali ina maslahi nayo.
"Katika kutekeleza majukumu hayo, Msajili Mkuu anasaidiwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Msajili wa Mahakama Kuu, Naibu Wasajili na Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri, Kurugenzi ya Huduma za Mahakama, Ukaguzi na usimamizi wa Maadili pamoja na Kurugenzi ya TEHAMA. Majukumu haya yamefafanuliwa kwa kina kwenye taarifa ya Makabidhiano nitakayokukabidhi hivi punde."amesema Jaji Chuma.
"Kwa ufupi, taarifa inaainisha maeneo mbalimbali ambayo yalikuwa yanaendelea kufanyiwa kazi na ofisi ya Msajili Mkuu. Miongoni mwa naeneo hayo kwa uchache ambayo pia ni mafanikio ya Mahakama kwa kipindi chote nilichohudumu ni"
"Kuendelea kusimamia mikakati ya kuiwezesha Mahakama kuondokana na mlundikano wa mashauri uliopungua kutoka 11% 2019 hadi asilimia 3 Machi, 2024"
Amesema majukumu aliyeendelea nayo ni kusimamia mfumo wa uratibu wa mashauri (Advanced Case Management System);
Kusimamia na kuratibu mfumo wa unukuzi na tafsiri yaani, transcription and translation system (TTs).
Jaji Chuma amesema kuwa majukumu anayotakiwa kuyavalua njuga ni pamoja na kuhakikisha maamuzi ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu yanapatikana katika mfumo wa TANZLII. Kutoka mwaka 2018 hadi sasa jumla ya maamuzi 50,505. Hapa kuna elimu ya kutosha kwa umma kupitia maamuzi haya;
Kuongezeka kwa idadi ya vituo vya Mahakama zinazokaguliwa kutoka 75.8% mwaka 2017 hadi 98.1% mwaka 2023, Kuendelea kupunguza hatua za kuendesha mashauri kwa maana procedural steps ambazo zilipungua kutoka hatua 38 hadi hatua 21.
Amesema kuwa utekelezaji wa maoni kuhusu ripoti ya REPOA ya mwaka 2023 ambayo kuridhika kwa umma juu ya huduma zinazotolewa na Mahakama iliongezeka kutoka asilimia 61% 2015 hadi 88% 2023.
"Lakini pia ni muhimu kulinda na kuendelea kuongeza asilimia kwa kuongeza uwajibikaji. Hii ni hatua kubwa japo wapo wanaobeza juhudi hizi. Lakini nao ni wetu na wanapaswa kuhudumiwa".
"Kuendelea kulinda uhuru wa Mahakama na kusimamia nidhamu kwa maafisa wa Mahakama" amesema Jaji Chuma.
Nkya Msajili Mkuu wa Mahakama akpoea majukumu ya Ofisi ya Msajili Mkuu wa Mahakama ameahidi kuwa atafanya jitihada zake zote kuhakikisha kuwa muhimli huo unazidisha kasi katika utoaji haki kwa wananchi.
Msajili Nkya amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kumuamini na kuahidi kuwa atatekeleza majukumu yake kadri ya uwezo wake wote.
Amesema kuwa amezipokea nasaha na ushauri wa Msajili Mkuu wa zamani "Nasaha zako ni nzuri zitaniimarisha ,niahidi kwamba nitatekeleza majukumu yangu kulingana na kiapo changu pia kwa uwezo ambao ungu ameniajaaliwa nitafanya kazi kadri ya uwezo wangu wa mwisho".
Msajili Nkya ameiomba ushirikino kwa watendaji na watumishi wote wa mahakama na kusisitiza kufanya kazi kwa jitihada zote kuhakikisha muhimili wa mahakama uzidi kuwa imara.
No comments:
Post a Comment