Kampuni kubwa ya mawasiliano
Halotel, inayoendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kwa
jamii, imejitolea kudhamini tukio la Iftar kwa uongozi wa mtaa wa
Bwawani na jamii ya watu wa Makumbusho kwa ujumla.
Halotel akiwa
ni mtoa huduma wa mawasiliano Tanzania, akitoa huduma mbalimbali za
mawasiliano na akiendelea kukidhi mahitaji ya wateja wao. Kwa kuzingatia
utoaji huduma bora na uaminifu Halotel inaendelea kutoa huduma bora na
kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya mawasiliano na jamii kiujumla.
Tukio
hili la Iftar linalenga kuileta pamoja jamii katika kipindi hiki cha
Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Halotel inaamini katika umoja na mshikamano
kama kauli mbiu ya kampuni inavosema ‘Pamoja kwa Ubora’ na tumeona ni
muhimu kusaidia juhudi za serikali kuleta watu pamoja na leo tupo tena
Makumbusho katika kukuza uhusiano mzuri wa jamii zinazotuzunguka.
Kwa
niaba ya Uongozi wa uongozi wa Bwawani, Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwawani
Ndugu Ismail Mwenda alishukuru kampuni ya Halotel Tanzania kuonesha nia
ya kuunganisha watu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. “Hii ni
chachu katika jamii kampuni inapoamua kuunganisha watu katika mwezi huu
mtukufu wa Ramadhani, inaonesha upendo na mshikamano kati ya watu wa
Makumbusho na jamii kiujumla” aliendelea kusema Ndugu Israel Mwenda.
“Katika
mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, Halotel kwa ushirikiano na Serikali
tunajivunia kuandaa iftar kwa ajili ya Jamii yetu” Aliongea Naibu
Mkurugenzi wa Fedha Halotel “Hii ni ishara ya Umoja wetu, mshikamano na
undugu unaotuunganisha sote. Ni wakati wa kushiriki, kusadiana na
kuimarisha mahusiano yetu katika jamii” alimalizia Ndugu Najib Ferej.
Kupitia
udhamini huu, tunawawezesha uongozi wa mtaa wa Makumbusho kufanya tukio
la Iftar kuwa la kipekee na la kumbukumbu kwa wakazi wa Makumbusho na
wafanyabiashara wadogowadogo wanaozunguka eneo hili. Halotel inatambua
umuhimu wa kujenga jumuiya zenye upendo na tunaamini kuwa tukio hili
litakuwa fursa nzuri ya kuimarisha mahusiano ya kijamii na kukuza
utamaduni.
Halotel haitoishia hapa katika kuweka mkono katika
jamii, tutaendelea kuweka nguvu katika kukuza umoja na mshikamano katika
jamii yetu vivo hivyo Halotel itaendelea kuboresha huduma zake ambazo
zinarahisisha mawasiliano mijini na kijijini.
Halotel
Tanzania yashirikiana na Uongozi wa mtaa wa Bwawani katika kufturisha
Mtaa wa Makumbusho. Tukio hili la Iftar limelenga kuongeza upendo na
Ushirikiano katika Jamii katika kipindi hiki cha Ramadhan.
Halotel Yatia mkono Uongozi wa mtaa wa Bwawani kupitia ufadhili wa Tukio la Iftar.
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
No comments:
Post a Comment