Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
ameagiza wakandarasi kukamilisha ujenzi Machi mwakani na kwa ubora
unaotakiwa. Ujenzi wa uwanja huo utakaogharimu zaidi ya sh. Bil. 60
utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 150, 000 kwa mwaka na utarahisisha
zaidi usafiri kwa wakazi na wageni.
Watu 120 wamepata ajira katika mradi huo ambapo wazawa wamekuwa 114.
Dkt.
Nchimbi ametoa maagizo hayo leo Aprili 15, 2024 wakati kiwaongoza
viongozi wa chama na serikali kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa
Ndege wa Sumbawanga kwenye ziara yake mkoani Rukwa.
Dkt. Nchimbi
ambaye ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri
Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla
pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya
kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe
na Ruvuma.
Lengo la ziara hiyo ni kuhuisha uhai wa chama,
kutatua kero za wananchi, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa
ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
Baada ya kumaliza katika
mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio
makubwa, itaendelea kesho katika Mkoa Mbeya na hatimaye katika mikoa ya
Njombe na Ruvuma.
DKT. NCHIMBI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA SUMBAWANGA
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
No comments:
Post a Comment