NAIBU Waziri wa Maji Mhe.Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amemuagiza Meneja wa Ruwasa wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Mhandisi Erwin Sizinga aweze kuhakikisha wanakamilisha ulazaji wa bomba wa umbali wa kilomita 2.8 ndani ya wiki moja ili wananchi wa Kata ya Ubiri na Ngulwi waweze kupata huduma ya maji safi na salama.
Kadhalika Mhandisi Mahundi amemuagiza
Mkandarasi anayejenga Mradi wa Maji wa Magamba ahakikishe anaongeza kasi
ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ili aweze kukamilisha kwa
wakati.
Mhandisi Mahundi ametoa maagizo hayo leo Januari 6 2024,
alipotembelea na kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji ya
Magamba na Mradi ya Maji Irente-Yoghoi-Ngulwi iliyopo Wilayani Lushoto
Mkoani Tanga.
"Ili wananchi elfu 30,835 wa maeneo ya Magamba,
Kwesimu, Bara, Jegestal, Kambi namba nne, Chakechake, Kitivo, Maguzoni,
Sinza, Lushoto Mjini, Mabwawani, Kipembe na Kialilo waweze kupata huduma
ya maji miradi hii inapaswa kukamilika kwa wakati"amesema Mhandisi
Mahundi
Naye Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Mhe. Shaban Shekilindi
ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza miradi ya maji
kwenye jimbo hilo huku akisema wananchi wengi watapata huduma ya maji
huku akiwasisitiza wakandarasi kukamilisha kwa wakati.

No comments:
Post a Comment