Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekabidhi ya
tuzo ya heshima kwa benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ikiwa ni ishara ya
kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha msimu wa 17 wa tuzo za
Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda (PMAYA) sambamba na kuchochea kasi
ya ukuaji wa sekta ya viwanda nchini kwa ujumla kupitia huduma zake za
kifedha. Benki ya NBC ni mdhamini mkuu wa tuzo hizo za kila mwaka kwa
mwaka wa pili mfululizo.
Rais Samia alikabidhi tuzo hiyo kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Bw Theobald Sabi wakati wa hafla ya
utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Tuzo za PMAYA huandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI)
zikilenga kutambua mchango wa sekta ya viwanda kiuchumi na kuchochea
ushindani wa utoaji huduma miongoni mwa viwanda hivyo.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Rais Samia pamoja nakuwapongeza wadhamini mbalimbali
wa tuzo hizo ikiwemo benki ya NBC, aliangazia masuala mbalimbali
yanayohusu mustakabali wa sekta viwanda nchini hususani suala la
upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika huku pia akionyesha kutambua
mchango na umuhimu wa huduma za kifedha katika kukuza ustawi wa sekta ya
viwanda na kuchochea ushindani katika soko la ndani na nje ya nchini.
“Najua
kuna changamoto ya upatikanaji wa dola lakini nashukuru kuona kwamba
kupitia jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanywa na wataalamu wetu wa
masuala ya fedha ndio zimetusaidia kukabiliana na changamoto ya
upatikanaji wa dola. Kwasasa tunaweza kutoa hadi dola milioni 2 kwa mtu
mmoja kwa siku kutoka kiwango cha utoaji wa dola laki 5 kwa mtu mmoja
kwa siku katika kipindi ambacho hali ilikuwa mbaya zaidi.’’ Alisema Rais
Samia huku akibainisha kuwa hatua hiyo ni kubwa ikilinganishwa na
baadhi ya mataifa jirani ambayo kwasasa yanashindwa kutoa hata dola laki
5 kwa mtu mmoja kwa siku.
Alisema hata hivyo serikali inafanya
jitihada mbalimbali kuhakikisha inaongeza upatikanaji wa dola nchini
ikiwemo kuhamasisha ongezeko la bidhaa zinazouzwa nje ya nchi hususani
kupitia mauzo ya bidhaa zinazozalishwa kupitia sekta za viwanda na
kilimo hususani kilimo cha mboga mboga (horticulture)
Awali
akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw
Theobald Sabi alisema benki hiyo imejipanga katika utoaji wa huduma na
fursa mbalimbali kwa wadau wa sekta ya viwanda nchini ikiwemo mikopo ya
aina zote hususani ile inayolenga kuongeza uzalishaji viwandani, huduma
za bima nak inga dhidi ya majanga na mabadiliko ya riba, huduma za
malipo ya ndani na nje ya nchi ikiwemo ukusanyajaji wa mapato ya
serikali pamoja na utoaji wa mikopo inayowezesha biashara za kimataifa
(International Trade Financing).
“Pamoja na huduma kibenki kwa
wadau wa viwanda, NBC kwasasa tunatekeleza mkakati wetu wa kukuza huduma
rasmi za kibenki kwa makundi maalumu ikiwemo wafanyabiashara wadodo na
wa kati (SMEs), wanawake pamoja na wajasiriamali,’’ alibainisha Sabi
Kwa
mujibu wa Sabi ushirikiano baina ya wadau wakubwa wa viwanda na makundi
hayo maalum utachochea zaidi kasi ya ukuaji wa Uchumi nchini kutokana
na muingiliano mkubwa baina yao.
Aidha Bw Sabi ambae pia ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) alitumia fursa hiyo
kuwasilisha kwa Rais Samia utayari wa taasisi zote wananchama wa umoja
huo katika kuhudumia sekta ya viwanda nchini huku akipongeza jitihada
mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuweka mazingira rafiki ya
biashara ili kufungua nchi kiuchumi na kuvutia uwekezaji.
“Jitihada
hizi za serikali zinazoonekana katika maeneo mengi ikiwemo utalii,
miundombinu, mauzo ya bidhaa za nje (Export), ukuaji wa sekta madini na
maeneo mengine mengi ni matunda ya juhudi hizo za serikali ambazo
zimezaa fursa kubwa kwa taasisi za fedha nchini…tunashukuru sana
Mheshimiwa Rais,’’ alipongeza Sabi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
CTI Bw Paul Makanza alionyesha kuguswa zaidi na ushirikiano uliopo
baina ya wadau wa viwanda nchini pamoja na serikali kama ilivyo pia
baina ya wadau hao na taasisi za fedha nchini huku kipekee akiipongeza
benki ya NBC kwa namna inavyoshirikiana na wadau hao kupitia huduma zake
pamoja na udhamini wa benki hiyo kwenye matukio mbalimbali
yanayoandaliwa na wadau hao ikiwemo Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda
(TIMEXPO) na tuzo za PMAYA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani (Kushoto) akikabidhi tuzo ya heshima na utambuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (katikati) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha msimu wa 17 wa tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda (PMAYA) sambamba na kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya viwanda nchini kwa ujumla kupitia huduma zake za kifedha. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo zilizoratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki ya NBC ni mdhamini mkuu wa tuzo hizo za kila mwaka kwa mwaka wa pili mfululizo. Kulia ni Mwenyekiti wa CTI Bw Paul Makanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) akionesha mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan (Kushoto) tuzo ya heshima na utambuzi wa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha msimu wa 17 wa tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda (PMAYA) sambamba na kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya viwanda nchini kwa ujumla kupitia huduma zake za kifedha. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo zilizoratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki ya NBC ni mdhamini mkuu wa tuzo hizo za kila mwaka kwa mwaka wa pili mfululizo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji (MB) (kushoto) akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha msimu wa 17 wa tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda (PMAYA) sambamba na kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya viwanda nchini kwa ujumla kupitia huduma zake za kifedha. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo zilizoratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki ya NBC ni mdhamini mkuu wa tuzo hizo za kila mwaka kwa mwaka wa pili mfululizo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Samia (pichani) pamoja nakuwapongeza wadhamini mbalimbali wa tuzo hizo ikiwemo benki ya NBC, aliangazia masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa sekta viwanda nchini hususani suala la upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika huku pia akionyesha kutambua mchango na umuhimu wa huduma za kifedha katika kukuza ustawi wa sekta ya viwanda na kuchochea ushindani katika soko la ndani na nje ya nchini.
Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (pichani) alisema benki hiyo imejipanga katika utoaji wa huduma na fursa mbalimbali kwa wadau wa sekta ya viwanda nchini ikiwemo mikopo ya aina zote hususani ile inayolenga kuongeza uzalishaji viwandani, huduma za bima nak inga dhidi ya majanga na mabadiliko ya riba, huduma za malipo ya ndani na nje ya nchi ikiwemo ukusanyajaji wa mapato ya serikali pamoja na utoaji wa mikopo inayowezesha biashara za kimataifa (International Trade Financing).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji (MB) (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Albert Chalamila (Kushoto), Mwenyekiti wa CTI Bw Paul Makanza (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda (PMAYA) zilizoratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) zilizofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo Bw. Elvis Ndunguru ( wan ne kushoto) wakifuatilia tuzo hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo Bw. Elvis Ndunguru (Kulia) wakibadilishana mawazo na baadhi ya wadau mbalimbali wa sekta ya viwanda wakati wa tuzo hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani (Katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji (MB) (wa pili kushoto walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Albert Chalamila (Kushoto), Mwenyekiti wa CTI Bw Paul Makanza (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) pamoja na washiriki mbalimbali wa tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda (PMAYA) zilizoratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) zilizofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wan ne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa tuzo hizo.












No comments:
Post a Comment