*Aahidi ushirikiano wa kutosha kufanikisha utendaji wa Mfuko
*Mkurugenzi Mkuu aweka wazi mafanikio na mikakati ya uboreshaji huduma
Na MWANDISHI WETU
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi.
Mwamini Malemi, amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Mfuko wa Taifa
wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam, na kuahidi kufanya kazi
kwa ushirikiano na Menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Mfuko.
Katika
ziara hiyo ya kikazi iliyofanyika tarehe 5 Desemba 2023, Bi. Malemi
alikutana na kuzungumza na wajumbe wa Menejimenti ya NSSF, ambapo pamoja
na mambo mengine alipokea taarifa ya utendaji kazi kutoka kwa
Mkurugenzi wa Mkuu, Bw. Masha Mshomba.
Taarifa ya NSSF
iliyowasilishwa na Bw. Mshomba ilionesha utendaji mzima wa Mfuko,
ikigusia uandikishaji wanachama, uchangiaji, uwekezaji pamoja na ulipaji
mafao. Aidha Bw. Mshomba alizungumzia kuhusu uboreshaji huduma kwa
wanachama, uboreshaji mifumo na namna wafanyakazi wanavyoshirikiana
katika kuhakikisha majukumu ya Mfuko yanakamilika.
Akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza na Menejimenti ya NSSF,
Bi. Mwamini alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini
na kumteua kushika nafasi hiyo, ambapo aliahidi kufanya kazi kwa
ushirikiano ili kuweza kufikia malengo na matarajio ya Mfuko.
Awali,
Bw. Mshomba alimueleza Mwenyekiti huyo matarajio ya Mfuko ikiwemo
kuendelea kuboresha huduma kwa wanachama kupitia njia mbalimbali ikiwemo
ya matumizi ya TEHAMA kwani hicho ndio kipaumbele muhimu cha NSSF.
Bw.
Mshomba alisema matarajio ya Mfuko ni kuona mwanachama baada ya
kustaafu na kuwasilisha taarifa zake zote zinazotakiwa kwa mujibu wa
Sheria analipwa stahiki zake ndani ya muda mfupi.
MWENYEKITI WA BODI YA NSSF AFANYA ZIARA YA KIKAZI MAKAO MAKUU YA NSSF
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
No comments:
Post a Comment