JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MAHAFALI YA 17 YA DIT YAFANA, DIT WAASWA KUENDELEA KUHAMASISHA SHUGHULI ZA KIBUNIFU

Share This

 

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo ametoa rai kwa uongozi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) kuendelea kuhamasisha shughuli za ubunifu, kuwaibua na kuwaendeleza wabunifu wengi zaidi ili, kwa kupitia bunifu zao, wachangie katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za jamii na maendeleo ya taifa kwa ujumla.


Hayo ameyasema leo Desemba 7, 2023 alipomuwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (MB) katika Mahafali ya kumi na saba (17) ya Duru ya kwanza ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Kampasi Kuu ya Dar es salaam, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa DIT iendelee kutambua, kujenga, kukuza na kuendeleza ubunifu nchini katika nyanja za Sayansi na Teknolojia.

Pia amewaasa kuendesha mashindano ndani ya taasisi ili kupata wabunifu mahiri ambao wamefanya vizuri katika ngazi mbalimbali.

Katika Mahafali hayo Profesa Carolyne Nombo ametoa tuzo kwa wabunifu wa teknolojia wanne ambao ni Maximilian Charles, Ebenezer Zacharia, Robart Nyamaka, Goodluck Disanula ambao walibuni mtambo wa kuchakata mafuta ya alizeti na Merkizedeki Method ambaye alibuni mfumo wa mita za maji za kieletroniki za watumiaji wengi (e-Water).

“Nikiri kwamba haya mnayofanya yanaendana na malengo ya Serikali katika kukuza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.” Amesema Profesa Carolyne Nombo

Amesema Wizara itaendelea kusimamia uendelezaji wa masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili kutoa fursa kwa wabunifu na wagunduzi mbalimbali kujitokeza, kuonesha bunifu na gunduzi zao kupewa fursa ya kuzitumia kusaidia jamii na kuwaendeleza ili kufikia hatua ya kuzibiasharisha.

Kwa Upande wa Mwenyekiti Wa Baraza La Taasisi Ya Teknolojia Dar Es Salaam (DIT), Dkt. Richard Masika amesema kuwaa changamoto viwanda kutokutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa DIT ambapo inawakosesha Wanafunzi kuto kuongeza uzoefu viwandani “Staff Industrial Attachment”

Amesema ni vigumu kupata wataalam wa viwandani kwaajili ya kujitolea kutoa uzoefu wao, bado mwamko wanafunzi wa DIT Pia ametoa rai kwa wataalamu hasa wabobezi kutoka viwandani pamoja na Alumni wa DIT kutoka sekta binafsi na umma kwenda DIT kufundisha na kutoa uzoefu wao wa viwandani kwa vitendo pamoja na mihandhara, ili kuwapa wanafunzi zana na ujuzi na umahiri utakaowaongezea ufanisi na tija waingiapo kazini na wanapojiajiri.

“Hii ni fursa, ruksa, mnakaribishwa na karibuni sana.”

Akizungumzia kuhusiana na idadi ya Wahitimu, Mkuu Wa Taasisi Ya Teknolojia Dar Es Salaam (Dit) Profesa Preksedis Marco Ndomba amesema

katika mahafali ya 17 duru ya Kwanza ya DIT Kampasi Kuu Dar es Salam jumla ya wahitimu 1225 wanaume (ME) 923 na Wanawake (KE) 302 wametunukiwa tuzo mbalimbali, Stashahada 596 (ME – 425, KE – 171), 8 Stashada ya juu wote ni wa kiume, Shahada ya kwanza, 592 (ME – 464, KE – 128) na Shahada ya Uzamili 29 (ME - 26, KE – 3).

“Idadi ya wahitimu wa kike ni sawa na asilimia 25. Kimsingi tunajivunia kuendelea kuongeza asilimia ya wahitimu wa kike mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, miaka mitatu iliyopita asilimia ya wahitimu wa kike ilikuwa 21. Haya ni matunda ya hamasa kubwa tunayoendelea kufanya na tunaamini asilimia hii itaendelea kupanda mwaka hadi mwaka.”







Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo akitembelea bunifu za wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya kumi na saba (17) ya Duru ya kwanza ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Kampasi Kuu ya Dar es salaam, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam.
Maandamano ya Kitaaluma.




Baadhi ya Wahitimu wakiwa katika Mahafali ya kumi na saba (17) ya Duru ya kwanza ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Kampasi Kuu ya Dar es salaam, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo akiwatunuku shahada wakati Mahafali ya kumi na saba (17) ya Duru ya kwanza ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Kampasi Kuu ya Dar es salaam, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam.

Wahitimu wakitoka mara baada ya kutunukiwa shahada yao wakati Mahafali ya kumi na saba (17) ya Duru ya kwanza ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Kampasi Kuu ya Dar es salaam, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad